Naamini tumekua pamoja tangu tulipoanza kukuletea makala za uchambuzi wa timu shiriki katika fainali za kombe la dunia 2018, ngoja ngoja imekwisha na sasa tunahesabu saa kadhaa kabla ya kipyenga cha kuanza kwa fainali hizo hakijapulizwa mjini Moscow nchini Urusi baadae hii leo.

Tunaendelea kulichambua kundi H ambalo ni la mwisho katika makundi ya manane yaliyosheheni timu 32 shiriki katika fainali za kombe la dunia mwaka huu, na leo ni zamu ya timu ya taifa ya Colombia ambayo imepangwa na mataifa ya Poland, Senegal na Japan

Iliwalazimu wachezaji wa timu ya taifa ya Colombia kupambana kikamilifu ili kuipata nafasi ya kushiriki fainali za kombe la dunia za mwaka huu, kupitia ukanda wa kusini mwa Amerika ambapo kuna mataifa yenye uwezo wa hali ya juu katika medani ya soka.

Ukanda wa Amerika ya kusini kulikua na kundi moja ambalo lilijumuisha mataifa yote ambayo yaliwania nafasi nne, na kuiepuka nafasi ya tano ambayo humlazimu muhusiska kucheza mchezo wa mtoano dhidi ya mshindi kutoka ukanda wa Oceania.

Katika mshike mshike wa kundi la Amerika ya kusini, Colombia walibahatika kuwa sehemu ya timu nne zilizofuzu moja kwa moja kwenye fainali za mwaka huu 2018.

Colombia walimaliza katika nafasi ya nne, kwenye msimamo wa kundi hilo baada ya kufikisha alama 27, wakitanguliwa na timu za mataifa ya Argentina, Uruguay na Brazil, huku Peru ikimaliza nafasi ya tano.

Majina ya utani ya timu ya taifa ya Colombia: Los Cafeteros (The Coffee Growers) na La Tricolor (The Tricolors).

Mfumo: Kikosi cha Colombia hutumia mfumo wa 4-2-3-1.

Image result for James Rodríguez - colombiaMchezaji Nyota: James Rodríguez (anacheza kwa mkopo FC Bayern Munich, akitokea Real Madrid)

Image result for Davinson Sánchez - colombiaMchezaji hatari: Davinson Sánchez (Tottenham Hotpsur)

Related imageNahodha: Radamel Falcao García Zárate (AS Monaco)

Image result for José Néstor Pékerman Krimen - colombiaKocha: José Néstor Pékerman Krimen (68), raia wa Argentina.

Ushiriki: Colombia imeshiriki fainali za kombe la dunia mara tano (05). Mwaka 1962, 1990, 1994, 1998, 1998 na 2014.

Mafanikio: Robo fainali (2014)

 

Kuelekea 2018:

Kikosi cha timu ya taifa ya Colombia kitahitaji kuvuka mafanikio ya kufika robo fainali kama walivyofanya mwaka 2014 wakiwa nchini Brazil chini ya kocha wao José Néstor Pékerman Krimen ambaye amedumu tangu wakati huo.

Katika fainali za 2014 walionyesha soka safi na kila shabiki duniani aliamini huenda wangevuka robo fainali kwa kuwaondoa wenyeji Brazil, lakini haikua hivyo.

Mwaka huu kocha José Néstor Pékerman Krimen, ameshaeleza wazi dhamira yake ya kuhakikisha mambo yanakua vizuri, hasa baada ya kuona mwenendo wa kufurahisha kwa wachezaji wake ambao wametapakaa katika ligi mbalimbali duniani.

“Hatua ya kufuzu kucheza fainali za 2018, ilikua ngumu kwetu, lakini tumefanikiwa kufaulu mtihani huu, ninaamini tunakwenda kushindana,”

“Dhamira yetu ni kuvuka hatua ya robo fainali ambayo tuliishia mwaka 2014, nimefuatilia mwenendo wa wachezaji wangu wakiwa katika klabu zao, nimefurahishwa na maendeeo yao, hivyo ninaamini kikosi kitakua katika hali nzuri ya kushindana tukiwa nchini Urusi.” Alizungumza kocha José Pékerman katika mkutano wake na waandishi wa habari siku za hivi karibuni.

Kikosi cha Colombia kina wachezaji wazuri na wenye uzoefu wa kutosha kama James Rodríguez, Radamel Falcao, Mlinda mlango David Ospina, Carlos Bacca, Luís Muriel, Miguel Borja, José Izquierdo, Avinson Sánchez, Yerry Mina, Cristián Zapata, Santiago Arias na Frank Fabra.

Colombia wataanza kampeni za kuusaka ubingwa wa mwaka huu kwa kucheza dhidi ya Japan, Uwanja wa Mordovia mjini SaranskJuni 19, kisha watapambana na Poland Juni 24, Uwanja wa Kazan mjini Kazan, na mchezo wao wa mwisho hatua ya makundi watakutana na Senegal Juni 28,uwanja wa  Cosmos mjini Samara.

Je, Colombia itaweza kuvuka lengo la kufika robo fainali katika fainali za mwaka huu? Tusubiri na kuona mana mchaka mchaka wa michuano hiyo inaanza leo nchini Urusi, Kaa hapa na Dar24 tukujuze, usipitwe kupitia YouTube Channel yetu ‘Dar24 Media’.

Salva Kiir, Machar uso kwa uso Ethiopia
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 14, 2018