Hispania ilifuzu kucheza fainali za kombe la dunia 2018, ikitokea ukanda wa barani Ulaya, ikiongoza msimamo wa kundi G (Kundi la 7), ambalo lilikua na timu za Italia, Albania, Israel, Macedonia na Liechtenstein.

Hispania walioweka historia ya kutwaa ubingwa wa Ulaya mwaka 2008 na kuutetea mwaka 2012, waliongoza msimamo wa kundi hilo kwa kufikisha alama 28, wakifuatiwa na Italia waliomaliza na alama 23.

Hatua ya kumaliza kinara wa kundi, moja kwa moja Hispania walikata tiketi ya kucheza fainali za 21 za kombe la dunia, ambazo zitaanza rasmi Juni 14, 2018 nchini Urusi.

Majina ya utani: La Furia Roja (The Red Fury), La Furia (The Fury) na La Roja (The Red).

Mfumo: Kikosi cha Hispania hutumia mfumo wa 4-5-1.

Image result for David SilvaMchezaji Nyota: David Silva (Manchester City).

Image result for iscoMchezaji hatari: Isco (Real Madrid).

Image result for Sergio RamosNahodha: Sergio Ramos García (Real Madrid)

Image result for Julen Lopetegui ArgoteKocha: Julen Lopetegui Argote (51), raia wa Hispania.

Ushiriki: Hispania wameshiriki fainali za kombe la dunia mara kumi na nne (14). Mwaka 1934, 1950, 1962, 1966, 1978, 1982, 1986, 1990, 1994, 1998, 2002, 2006, 2010 na 2014. Hii ni mara ya 15. Hivyo, Inaweka historia nzuri ya kushiriki michuano 15 kati ya 21 ya fainali hizo.

Mafanikio: Ni moja kati ya timu nane zilizowahi kutwaa Kombe la Dunia, ilitwa ubingwa mwaka 2010, nchini Afrika Kusini. Imefika robo fainali mara nne. Mwaka 1950 ilishika nafasi ya nne.

Kuelekea 2018:

Baada ya kuondolewa katika hatua ya makundi wakati wa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 zilizofanyika nchini Brazil, Hispania imejipanga kikamilifu ili isirudie makosa hayo ikitafuta kurudia historia nzuri ya mwaka 2010.

Mwaka huu imejiandaa kwa kuwa na kikosi chenye wachezaji wengi chipukizi, ambao baadhi yao walianza kuonekana wakati wa fainali za Ulaya za 2016 zilizofanyika Ufaransa.

Asilimia kubwa ya wachezaji chipukizi wa taifa la Hispania lenye watu zaidi ya 46,354,321, waliunda kikosi cha nchi hiyo kilichotwaa ubingwa wa michuano ya vijana ya Ulaya chini ya miaka 21 ya mwaka 2013.

Baadhi yao ni Nacho, Marc Bartra, Iñigo Martínez, Sergio Canales, Koke, Rodrigo Moreno, Thiago Alcântara, Cristian Tello, Álvaro Morata, Diego Mariño, Ignacio Camacho, Marc Muniesa, Álvaro González, Pablo Sarabia, Alberto Moreno, Iker Muniain, Dani Carvajal na  Álvaro Vázquez, Isco.

Kwa upande wa wachezaji wazoefu ambao wataunda kikosi cha mwaka huu 2018, yupo David De Gea, Gerard Piqué, Sergio Ramos, Jordi Alba, Sergio Busquets, David Silva na Álvaro Morata.

Hispania itaanza kampeni za kuusaka ubingwa mwaka huu kwa kucheza dhidi ya Ureno, Uwanja wa Fisht Olympic, mjini Sochi Juni 15, kisha watapambana na Iran Juni 20, Uwanja wa Kazan mjini Kazan, na mchezo wao wa mwisho katika hatua ya makundi watapapatuana na Morocco Juni 25 katika Uwanja wa Kaliningrad, mjini Kaliningrad.

Ni David Silva (Manchester City) na Isco (Real Madrid) ndio wanaotarajiwa kuibeba zaidi Hispania kuhakikisha inarudi nyumbani na Kombe.

Wachezaji hawa wawili wamekua na msimu mzuri katika klabu zao japo upande wa Real Madrid hawakufanya vyema katika ligi ya nchini Hispania.

Isco na Silva wamefanikisha malengo ya mameneja wa klabu za Man City na Real Madrid, jambo ambalo linaaminiwa juhudi zao wakizionyesha upande wa timu ya taifa ya Hispania zitazaa matunda na kuifikisha mbali timu yao.

Serikali yawaweka mtegoni wafanyabiashara ya watu
Chanjo ya Ebola yaanza kutolewa nchini Congo DR

Comments

comments