Siku, saa na dakika zinazidi kutusogeza kwenye kipyenga cha kwanza cha fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi mwaka huu. Dar24 tunaendelea kutekeleza ahadi yetu ya kukumulikia kila timu ya taifa iliyofuzu, na leo tunaimulika Iceland iliyopangwa Kundi D.

Iceland iko katika Kundi D na timu za taifa za Argentina, Croatia na Nigeria.

Ilifuzu fainali za kombe la dunia 2018, ikitokea ukanda wa barani Ulaya, baada ya kuongoza kundi la 9 (kundi I) lililokuwa na mataifa ya Croatia, Ukraine, Turkey, Finland na Kosovo.

Iceland walikata tiketi ya moja kwa moja kwa kufikisha alama 22, wakifuatiwa na  Croatia (alama 20), Ukraine (alama 17), Turkey/Uturuki (alama 15), Finland (alama 9) na  Kosovo waliburuza mkia wa kundi hilo kwa kuwa na alama moja.

Jina la utani la timu ya taifa ya Iceland: Strákarnir okkar (Our Boys)

Mfumo: Kikosi cha Iceland hutumia mfumo wa 4-4-2 / 4-5-1.

Image result for Gylfi Sigurdsson - icelandMchezaji Nyota: Gylfi Sigurdsson (Everton)

Related imageMchezaji hatari: Hordur Bjorgvin Magnusson (Bristol City).

Image result for Aron Einar Malmquist Gunnarsson - icelandNahodha: Aron Einar Malmquist Gunnarsson (Cardiff City).

Image result for Heimir Hallgrimsson - icelandKocha: Heimir Hallgrimsson (50), raia wa Iceland.

Ushiriki: Iceland haijawahi kushiriki fainali za kombe la dunia.

 

Kuelekea 2018:

Huenda taifa hili likawa na mashabiki wachache zaidi wakati wa fainali za kombe la dunia 2018, hii ni kutokana na nchi ya Iceland kuwa na idadi ndogo ya watu, yaani 350,710.

Wakati wa fainali za Ulaya 2016, Iceland ilikuwa na asilimia 10 ya mashabiki waliokwenda kuzishangilia timu zao nchini Ufaransa.

Katika Fainali za Ulaya 2016, timu ya taifa ya Iceland iliwashangaza mashabiki wengi wa soka ulimwenguni, kwa kufika hatua ya robo fainali, huku wakiitoa Uingereza kwenye mchezo wa mtoano (16 Bora).

Kutokana na mafanikio hayo, Iceland wanapewa nafasi kubwa ya kuendelea kuushangaza ulimwengu. Timu hii ina kikosi chenye kujituma bila kuhofia mataifa yenye majina makubwa katika soka.

Jambo kubwa ni kusubiri na kuona kama Iceland watafanikiwa kufika mbali kwenye fainali za kombe la dunia 2018, na ikiwezekana kutwaa ubingwa kwa mara ya kwanza.

Iceland wataanza kampeni za kuusaka ubingwa mwaka huu kwa kucheza dhidi ya Argentina, Uwanja Otkritie, mjini Moscow, Juni 16, kisha watapambana na Nigeria Juni 21, Uwanja wa Volgograd, mjini Volgograd, na mchezo wao wa mwisho hatua ya makundi watakutana na Croatia Juni 26, Uwanja Rostov, mjini Rostov-on-Don.

Kuwa na idadi ndogo ya watu sio hoja tena, Iceland inaonesha kuwa ina watu wachache lakini wenye nguvu na moyo wa ziada wa kujituma katika kila wanachokitafuta. Sasa wanalitafuta Kombe la Dunia la Fifa mwaka huu. Je, watalinyanyua? Mwamuzi dakika 90 za kila mchezo.

Kesho tutaendelea kumulika timu za kundi hili, kaa hapa, mwalike rafiki amualike rafiki. Usisahau kutembelea YouTube Channel yetu ‘Dar24 Media’, tunakusogeza Urusi.

 

Cristiano Ronaldo aendelea kuwavuruga mashabiki
Wanakijiji wauawa kikatili Msumbiji

Comments

comments