Mexico inaingia kwenye mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia ikiwa na historia nzuri. Kikosi hiki kimepangwa kwenye kundi E, pamoja na Ujerumani, Sweden na Korea Kusini.

Mexico ilifuzu fainali za kombe la dunia za mwaka huu ikitokea ukanda wa Amerika ya Kati na Kaskazini (CONCACAF).

Kikosi hiki kilianza harakati zake za kuwania kufuzu fainali hizo katika mzunguuko wa nne wa ukanda huo kwa kushiriki michezo ya kundi A (Kundi La Kwanza) lililokuwa na timu za mataifa ya Honduras, Canada na El Salvador.

Katika michezo ya kundi hilo, Mexico haikupoteza mchezo hata mmoja, zaidi ya kuambulia matokeo ya sare ya bila kufungana dhidi ya Honduras, hatua mbayo ililiwezesha taifa hilo kumaliza kinara wa kundi kwa kufikisha alama 16 na kufunzu hatua ya tano ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia.

Katika hatua hiyo Mexico ilipangwa tena katika kundi moja lililokuwa na timu za mataifa zilzioongoza misimamo ya makundi ya hatua ya nne ambazo ni Costa Rica, Panama, Honduras, Marekani (USA) na Trinidad & Tobago.

Bado Mexico ilikuwa moto, kwani iliendelea kuvuruga na kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika kundi hilo kwa kufikisha alama 21 ambazo ziliwavusha na kuwapatia tiketi ya kushiriki fainali za kombe la dunia.

Majina ya utani ya timu ya taifa ya Mexico: El Tri (The Tri) na El Tricolor (The Tricolor)

Mfumo: Kikosi cha Mexico hutumia mfumo wa 5-4-1.

Image result for Javier “Chicharito” Hernández - mexicoMchezaji Nyota: Javier “Chicharito” Hernández (West Ham United)

Image result for Hirving “Chucky” Lozano - mexicoMchezaji hatari: Hirving “Chucky” Lozano (PSV Eindhoven).

Image result for José Andrés Guardado Hernández - mexicoNahodha: José Andrés Guardado Hernández (Real Betis)

Image result for Juan Carlos Osorio Arbeláez - mexicoKocha: Juan Carlos Osorio Arbeláez (56), raia wa Colombia.

Ushiriki: Mexico imeshiriki fainali za kombe la dunia mara kumi na tano (15). Mwaka 1930, 1950, 1954,1958,1962,1966, 1970, 1978,1986,1994, 1998, 2002, 2006, 2010 na  2014. Mwaka huu ni mara ya 16.

Mafanikio: Robo fainali (1970 na 1986).

Kuelekea 2018:

Tangu mwaka 2015 kikosi cha Mexico kilipoanza kunolewa na kocha Juan Carlos Osorio, kimekuwa na matokeo ya kuridhisha, kilivyoanza kampeni ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka huu, mashabiki hawakuwa na wasiwasi wowote.

Umaridadi na ujasiri wa baadhi ya wachezaji wa Mexico ndio unaipa ushujaa timu ya taifa hilo ambalo limekuwa halina bahati pindi linaposhiriki fainali za kombe la dunia.

Uwepo wa mlinda mlango mashuhuri Guillermo Ochoa na wachezjai wengine Andrés Guardado, Héctor Moreno, Héctor Herrera na Javier Hernández ulimuwezesha kocha Osorio kufanya kazi yake kwa utaratibu na kufikia lengo la kuipeleka Mexico katika fainali za kombe la dunia.

Utumiaji wa mfumo wa 4-3-3 wa kocha huyo, nao ulikuwa chachu ya Mexico kupata mafanikio ya kufuzu fainali za kombe la dunia, na bado anatarajiwa kutumia mfumo huo wakati wa fainali zitakazoanza Juni 14 nchini Urusi.

Mexico wataanza kampeni za kuusaka ubingwa wa mwaka huu kwa kucheza dhidi ya Ujerumani, Uwanja wa Luzhniki mjini Moscow Juni 17, kisha watapambana na Korea Kusini Juni 23, Uwanja wa Rostov, mjini Rostov-on-Don, na mchezo wao wa mwisho hatua ya makundi watakutana na Sweden Juni 27, Uwanja Central mjini Yekaterinburg.

Jabali hili la Soka linatarajiwa kuleta ushindani mkubwa kwenye fainali za mwaka huu. Lakini lolote linaweza kutokea kipyenga kinapopulizwa. Endelea kuifuatilia Dar24 tukujuze na kukusogeza Urusi. Kesho tutamulika kikosi kingine cha Timu ya Taifa inayoelekea Urusi katikati ya Juni. Kaa nasi.

Tembelea Channel yetu ya YouTube ‘Dar24 Media’ kupata mengi zaidi.

Live: Mazishi ya Maria na Consolata mkoani Iringa
Video: Billnass aapa kufanya maajabu CCM Kirumba katika Sports & Music Festival 2018