Katika kuendelea kuzimulika timu zinazoshiriki Fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi mwezi ujao, tunaendelea na timu zilizopangwa Kundi B, ambazo ni Ureno, Hispania, Morocco, na Iran. Leo tunaimulika Ureno.

Morocco ilifuzu fainali za mwaka huu, ikitokea barani Afrika kwa kuongoza kundi C (Kundi la tatu) lililokuwa na timu za Ivory Coast, Gabon na Mali.

Ilimaliza kinara katika kundi hilo kwa kufikisha alama 12, ikifuatiwa na Ivory Coast waliopata alama 8, Gabon nafasi ya tatu kwa kuwa na alama 6 huku Mali wakiburuza mkia kwa kufikisha alama 4.

Jina la utani la timu ya taifa ya Morocco: Simba wa Atlas (Lions of the Atlas).

Mfumo: Kikosi cha Morocco hutumia mfumo wa 4-5-1.

Image result for Hakim ZiyechMchezaji Nyota: Hakim Ziyech (Ajax).

Image result for Sofiane BoufalMchezaji hatari: Sofiane Boufal (Southampton).

Image result for Medhi BenatiaNahodha: Medhi Benatia (Juventus)

Image result for Hervé RenardKocha: Hervé Renard Kocha Hervé Renard (49), raia wa Ufaransa.

 

Ushiriki: Morocco wameshiriki fainali za kombe la dunia mara tano (5). Mwaka 1970, 1986, 1994, 1986 na 1998.

Mafanikio: Hatua ya Mtoano (16 Bora mwaka 1986).

 

Kuelekea 2018:

Timu yataifa ya Morocco imerejea tena katika fainali za kombe la dunia, baada ya miaka 20 kupita, kwa mara ya mwisho walishiriki mwaka 1998 nchini Ufaransa.

Morocco, ni taifa pekee kutoka barani Afrika lililofuzu fainali za kombe la dunia bila kuruhusu bao wakati ikipocheza dhidi ya Ivory Coast, Gabon na Mali (Michezo ya nyumbani na ugenini), hatua hiyo ilitokana na kuwa na na safu nzuri na kali ya ulinzi.

Safu ya ulinzi ya taifa hili la kaskazini mwa Afrika lenye watu zaidi ya 33,848,242, inaundwa na wachezjai wenye uzoefu kama Karim El Ahmadi, M’barek Boussoufa na Mehdi Benatia wa klabu bingwa nchini Italia Juventus.

Kiungo Hakim Ziyech na mshambuliaji wa pembeni Nordin Amrabat wamekua chachu ya kuwapa jeuri mashabiki wa Morocco, kutokana na soka safi wanalocheza, hivyo wanatarajiwa kuendeleza moto wao wakati wa fainali za kombe la dunia nchini Urisi.

Kocha Hervé Renard anategemea sana ushauri na mawazo kutoka kwa wasaidizi wake Patrice Beaumelle na gwiji klabu ya Coventry City pamoja na timu ya taifa ya Morocco Mustapha Hadji, kutimiza lengo la kuushangaza Ulimwengu.

Morocco itaanza kampeni za kuusaka ubingwa mwaka huu kwa kucheza dhidi ya Iran, Uwanja wa Krestovsky mjini Saint Petersburg Juni 15, kisha watapambana na Ureno Juni 20 Uwanja wa Luzhniki mjini Moscow, na mchezo wao wa mwisho hatua ya makundi watapapatuana na Hispania Juni 25, Uwanja Kaliningrad, mjini Kaliningrad.

R. Kelly abanwa tena kwa unyanyasaji wa kingono
Miguna amvimbia Odinga