Peru imeingia kwenye mtanange wa Fainali za Kombe la Dunia baada ya kutofanikiwa kwa zaidi ya miaka 35. Wametumbukizwa kwenye chungu cha cha kundi C chenye wababe wengine ambao ni Ufaransa, Australia, Peru na Denmark.

Safari ya kufuzu:

Haikua kazi rahisi kwa Peru kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka huu, baada ya taifa hilo la Amerika Kusini kumaliza katika nafasi ya tano, kwenye msimamo wa kundi la ukanda huo.

Nafasi za ushiriki wa fainali za kombe la dunia katika ukanda wa Amerika ya Kusini zilikuwa zikiwaniwa na mataifa ya Colombia, Chile, Paraguay, Argentina, Brazil, Ecuador, Venezuela, Bolivia, Peru na Uruguay.

Peru ilimaliza kwenye nafasi ya tano kwa kujikusanyia alama 26, sawa na Chile, lakini Peru ilinufaika na tofauti ya bao moja la kufunga na kufungwa, hivyo ikajikatia tiketi ya kwenda kucheza mchezo wa mtoano dhidi ya mshindi kutoka ukanda wa Oceania (New Zealand).

Mchezo wa mkondo wa kwanza dhidi ya New Zealand ulichezwa Westpac Stadium, mjini Wellington, wenyeji walishindwa kufurukuta na kujikuta wakilazimishwa matokeo ya bila kufungana dhidi ya Peru.

Mchezo wa mkondo wa pili uliochezwa Estadio Nacional, mjini Lima, Peru walitumia vizuri nafasi ya kucheza nyumbani, kwa kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri, na kukata tiketi ya kucheza fainali za kombe la dunia.

Majina ya utani ya timu ya taifa ya Peru: La Blanquirroja (The White and Red) na Los Incas (The Incas)

Mfumo: Kikosi cha Peru hutumia mfumo wa 4-2-3-1.

Image result for Jefferson FarfánMchezaji Nyota: Jefferson Farfán (Lokomotiv Moscow).

Image result for Christian CuevaMchezaji hatari: Christian Cueva (São Paulo).

Related imageNahodha: Alberto Junior Rodríguez (Atlético Junior)

Image result for Ricardo Alberto Gareca NardiKocha: Ricardo Alberto Gareca Nardi (60), raia wa Argentina.

Ushiriki: Peru imeshiriki fainali za kombe la dunia mara nne (4). Mwaka 1930, 1970, 1978 na 1982.

Mafanikio: Kufika hatua ya robo fainali (1970).

Kuelekea 2018:

Peru wanarejea katika fainali za kombe la dunia kwa mara ya kwanza, baada ya miaka 36.

Sifa na pongezi zinapaswa kupelekwa kwa kocha wa kikosi hichio, Ricardo Gareca ambaye amelikomboa taifa hiyo kwa kurejea kwenye ramani ya soka la dunia.

Kocha huyo raia wa Argentina alionesha kuwaamini sana wachezaji chipukizi ambao mara kwa mara aliwaita kikosini kwake kwa ajili ya michezo ya kuwania kufuzu fainali za 2018.

Mfumo wa kupiga pasi nyingi na kushambulia kwa kasi, kuliisaidia Peru kufikia lengo la kupata tiketi ya kushiriki fainali hizo, baada ya miaka 36 kupita.

Wachezaji Pedro Gallese (Mlinda Mlango) leader Alberto Rodríguez (Beki) Yoshimar Yotún (Beki wa pembeni), Jefferson Farfán (Kiungo), mshambuliaji Paolo Guerrero, Mshambuliaji wa pembeni Aldo Corzo, beki wa kushoto Miguel Trauco na kiungo mshambuliaji Christian Cueva wanategemewa sana na mashabiki wa soka nchini Peru, huku wakiaminiwa kupeleka maajabu katika fainali za Urusi.

Peru itaanza kampeni za kuusaka ubingwa mwaka huu kwa kucheza dhidi ya Denmark, Uwanja Mordovia, mjini Saransk, Juni 16, kisha watapambana na Ufaransa Juni 21, Uwanja wa Central, Yekaterinburg, mjini Samara, na mchezo wao wa mwisho hatua ya makundi watakutana na Australia Juni 26, Uwanja Fisht Olympic, mjini Sochi.

Vidole vya raia wa Peru na mashabiki wake duniani kote vinakunjwa ili timu hiyo iandike historia ya kurejea kwa kishindo. Je, watavuna mbivu au mbichi? Zimebaki siku chache kuufyeka msitu.

Endelea kufuatilia makala hizi fupi. Pia, tembelea YouTube Channel yetu ya Dar24 Media kupata mengi yanayofurahisha, kuelimisha na kuhabarisha.

Magazeti ya Tanzania leo Mei 27, 2018
Samia Suluhu awataka TAWLA kuwasaidia wanawake wajasilia mali