Leo tunakamilisha uchambuzi wa kundi E tukiimulika Serbia ambayo itaanza kufurukuta ikiwa katikati ya miamba Brazil, Uswisi na Costa Rica.

Serbia ilifuzu fainali za kombe la dunia ikitokea ukanda wa barani Ulaya (UEFA), kwa kuongoza msimamo wa kundi D (Kundi la Nne) lililokuwa na timu za Jamhuri ya Ireland, Wales, Austria, Georgia na Moldova.

Serbia ilifanikiwa kupata alama 21, ambazo ziliivusha moja kwa moja hadi kwenye fainali za mwaka huu ambazo zinatarajiwa kuwa na upinzani mkali.

Majina ya utani ya timu ya taifa ya Serbia: La Sele (The Selection), La Muerte (Death), La Tricolor (The Tricolor) na Los Ticos (The Ticos)

Mfumo: Kikosi cha Serbia hutumia mfumo wa 3-4-3.

Image result for Nemanja Matic - serbiaMchezaji Nyota: Nemanja Matic (Manchester United)

Image result for Sergej Milinkovic-Savic - serbiaMchezaji hatari: Sergej Milinkovic-Savic (Lazio).

Related imageNahodha: Aleksandar Kolarov (AS Roma) 

Image result for Mladen Krstajić - serbiaKocha: Mladen Krstajić (44), raia wa Serbia.

Ushiriki: Serbia imeshiriki fainali za kombe la dunia mara kumi na moja (11). Mwaka 1930 (kama Kingdom of Yugoslavia), 1950, 1954, 1958, 1962, 1974, 1982, 1990, 1998 (SFR Yugoslavia), 2006 (Serbia na Montenegro) na 2010 (Serbia).

Mafanikio: Mshindi wa nne (1962).

Kuelekea 2018:

Serbia imefikia mafanikio hayo na kuweka rekodi ya kupambana ndani ya miaka saba baada ya kucheza fainali za mwaka 2010 nchini Afrika Kusini.

Mapambano ndani ya miaka saba yameiwezesha nchi hiyo ya Ulaya ya Mashariki kushiriki fainali za Ulaya za 2016 zilizochezwa nchini Ufaransa na kufika katika hatua ya nusu fainali.

Hali hiyo inatajwa iliwaongezea chachu wachezaji wa Serbia na kuingia katika mchakato wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia wakiwana morari ya hali ya juu kwa lengo la walifanikiwa kuivusha nchi yao.

Kikosi cha Serbia kilipoteza mchezo mmoja katika michezo 10 waliocheza ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia, jambo ambalo linaendelea kudhihirikisha ukali wake.

Kocha Slavoljub Muslin alifanikiwa kuendelea na kibarua chake kwa mafanikio alioyapata baada ya kuwa shakani kwa miezi kadhaa huku sababu nyingine ikitajwa kuwa ni ugomvi uliokuwepo baina yake na Rais wa Shirikisho la Soka la Serbia, Slavisa Kokeza.

Wawili hao walifikia hatua ya kutokuwa na mahusiano mazuri kufuatia Rais wa shirikisho la soka nchini Serbia kupinga mfumo wa kocha Muslin, ambao hakuamini kama ungeweza kuwavusha na kuwapelekea nchini Urusi.

Kwa kumtumia kiungo Sergej Milinkovic-Savic, kocha Muslin aliweza kumnyamazisha Rais huyo, na hivi sasa wamerejesha uhusiano mzuri.

Hata hivyo, baadaye kibarua cha Muslin kiliota nyasi kwa maamuzi ya mwisho yaliyofanywa na kamati ya utendaji ya shirikisho la soka nchini humo na nafasi yake ikachukuliwa na Mladen Krstajić.

Krstajić alikabidhiwa jukumu la kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Serbia Oktoba 2017, na anakumbukwa na mashabiki wengi wa soka nchini humo kufuatia mchango wake alioutoa akiwa kama mchezaji wakati wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2006.

Lakini bado maswali yanaendelea vichwani mwa mashabiki wa Serbia, ‘je, ni kweli Mladen Krstajić anatosha katika nafasi ya kukiongoza kikosi chao kwenye fainali za kombe la dunia nchini Urusi?”

Mimi na wewe tusubiri na kuona kama Mladen Krstajić kama atafanikiwa.

Serbia wataanza kampeni za kuusaka ubingwa mwaka huu kwa kucheza dhidi ya Costa Rica, Uwanja wa Cosmos, mjini Samara Juni 17, kisha watapambana na Uswiz Juni 22, Uwanja wa Kaliningrad mjini Kaliningrad, na mchezo wao wa mwisho hatua ya makundi watakutana na Brazil Juni 27, Uwanja Otkritie mjini Moscow.

Kwa mtazamo huo, kikosi cha Serbia kina matumaini ya kuwashangaza wadau wa soka duniani ingawa kiko kati kati ya msitu wa wababe wa soka.

Endelea kuwa na Dar24 tukusogeze karibu na Urusi. Kesho tunaanza kundi jipya lenye wababe waliopania kubeba kombe pia. Usikose kufuatilia channel yetu ya YouTube ‘Dar24 Media’ na kama bado huja-subscribe fanya hivyo leo.

Kocha Age Hareide amtema Nicklas Bendtner
Frederico Rodrigues de Paula Santos (Fred) kutua Old Trafford