Leo tumeanza kulimulika kundi C ambalo lina mabeberu wa soka ambao ni Ufaransa, Australia, Peru na Denmark. Kwa kuanza tunaanza na Ufaransa wenye historia ya aina yake kwenye mashindano haya.

Kikosi cha Ufaransa kilifanikiwa kufuzu Fainali za Kombe la Dunia kikitokea ukanda wa bara la Ulaya, kwa kuongoza kundi A lililokuwa na timu za Sweden, Uholanzi, Bulgaria, Luxembourg na Belarus.

Ufaransa iliongoza kundi hili kwa kufikisha alama 23 ambazo hazikuweza kufikiwa na timu nyingine, huku ikifuatiwa na Sweden waliomaliza na alama 19 sawa na Uholanzi, timu hizi mbili zilitofautishwa na mabao ya kufunga na kufungwa.

Nafasi ya nne katika kundi hilo ilikwenda kwa Bulgaria waliopata alama 13, wakifuatiwa na Luxembourg alama 6 na Belarus alama 5.

Majina ya utani: Les Bleus (The Blues) na Les Tricolores (The Tri-colours)

Mfumo: Kikosi cha Ufaransa hutumia mfumo wa 4-4-2 au 4-3-3.

Image result for Antoine Griezmann - FRANCEMchezaji Nyota: Antoine Griezmann (Atlético Madrid).

Image result for Kylian Mbappé  - FRANCEMchezaji hatari: Kylian Mbappé (Paris St-Germain).

Related imageNahodha: Hugo Lloris (Tottenham Hotspur)

Image result for Didier Claude Deschamps - franceKocha: Didier Claude Deschamps (49), raia wa Ufaransa.

 

Ushiriki: Ufaransa imeshiriki fainali za kombe la dunia mara kumi na nne (14). Mwaka 1930, 1934, 1938, 1954, 1966, 1978, 1982, 1986, 1998, 2006, 2010 na 2014. Hivyo, ilikuwa timu mojawapo kati ya timu nne za Ulaya zilizoshiriki mashindano ya kwanza ya Kombe la Dunia.

Mafanikio: Kutwaa Ubingwa mwaka 1998, ikiwa mwenyeji. Pia, mwaka 2006 waliingia fainali na kupoteza kwa mikwaju ya penalti 5-3 dhidi ya Italia.

Mwaka 1958 na mwaka 1986, Ufaransa ilifishika nafasi ya mshindi wa tatu katika fainali za Kombe la Dunia.

Kuelekea 2018:

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps ni amewahi kutoa kauli ambayo inaiweka timu hiyo nyuma ya matumaini makubwa yanayowekwa kwa tumi nyingine. Anaonesha kutofikiria sana kulitwaa taji la mwaka huu kwani anaamini miamba iliyoko mbele yao haichezi soka la aina yao.

Kocha huyo amewahi kukaririwa akisema, “hatupaswi kulinganishwa na Ujerumani, Hispania wala Brazil.”

“Hatujafikia katika viwango vya timu hizo kwa sababu sisi tunacheza soka la aina tofauti na wao, hivyo halitokuwa jambo la busara kama hatutafikiriwa katika hatua za juu zaidi.”

Didier Deschamps alikuwa ana maanisha timu yake ya Ufaransa haina sababu ya kupewa matumaini makubwa ya kutwaa ubingwa, zaidi ya kwenda Urusi kupambana na timu pinzani, na ikitokea wanafika mbali itakuwa ni kama bahati yao.

Lakini maneno hayo yamechukuliwa na baadhi ya wadadisi wa soka duniani, kama sehemu ya kujihami kwa kocha huyo ambaye alikiongoza kikosi cha Les Bleus mwaka 1998 kama nahodha na kutwaa ubingwa katika ardhi ya nyumbani kwao.

Pamoja na kutotaka kufananishwa na mataifa makubwa kisoka duniani, Deschamps ana haki ya kujivunia kuwa na safu bora ya ushambuliaji ambayo ina wachezaji kama Antoine Griezmann, Kylian Mbappé na Ousmane Dembélé.

Pia, ana wachezaji wazuri wanaocheza nafasi ya kiungo kama Paul Pogba na N’Golo Kanté, hivyo hapaswi kubezwa kama yeye alivyonukuliwa katika moja ya mikutano yake na waandishi wa habari, akitaka Ufaransa ichukuliwe kama timu inayokwenda kushiriki.

Ufaransa itaanza kampeni za kuusaka ubingwa mwaka huu kwa kucheza dhidi ya Australia, Uwanja wa Kazan, mjini Kazan Juni 16, kisha watapambana na Peru Juni 21, Uwanja wa Central, mjini Yekaterinburg, , na mchezo wao wa mwisho hatua ya makundi watakutana na Denmark Juni 26, Uwanja Luzhniki, mjini Moscow.

Tutaendelea kukumulikia timu za kundi C katika makala hizi fupi kumulika timu zinazokwenda Ufaransa kuwania nafasi ya kubeba Kombe la Dunia mwaka huu. Usiache kutembelea YouTube Channel yetu ya Dar24 Media kupata mengi usiyoyapata kwingineko.

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Mei 25, 2018
Video: Iliwauma sana ACT- Wazalendo baada ya kuwaaga- Prof. Kitila