Kabla ya kulimulika kundi hili jipya, yaani kundi F, tukutakie siku njema ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani. Bila mazingira bora hakutakuwa na soka. Mazingira ni maisha.

Turejee tena kwenye kundi hili, leo tunamulika kundi E ambalo lina timu za Ujerumani, Mexico, Sweden na Korea Kusini. Tunaanza na Ujerumani, wababe kwenye kilinge cha Kombe la Dunia. Ni mabingwa watetezi wanaingia kwenye mashindano ya mwaka huu kifua mbele.

Ujerumani ilifuzu fainali za kombe la dunia za 2018 ikitokea ukanda wa bara la Ulaya (UEFA), baada ya kuongoza msimamo wa kundi C (Kundi la Tatu) lililokuwa na na timu za mataifa ya Ireland ya Kaskazini, Czech Jamuhuri ya Czech, Norway, Azerbaijan na San Marino.

Ujerumani ilicheza michezo 10 ya kuwania kufuzu kupitia kundi hilo na ilishinda michezo yote na kujizolea alama 30.

Ilikuwa ni mafanikio makubwa kwa taifa hilo ambalo ndio bingwa mtetezi wa kombe la dunia, chini ya kocha Joachim Löw.

Majina ya utani ya timu ya taifa ya Ujerumani: Nationalelf (national eleven), DFB-Elf (DFB Eleven) na Die Mannschaft (The Team)

Mfumo: Kikosi cha Ujerumani hutumia mfumo wa 4-2-3-1.

Image result for Toni Kroos - germanyMchezaji Nyota: Toni Kroos (Real Madrid)

Image result for Leon Goretzka - germanyMchezaji hatari: Leon Goretzka (Schalke).

Image result for Manuel Neuer - germanyNahodha: Manuel Neuer (FC Bayern Munich) 

Image result for Joachim Löw - germanyKocha: Joachim Löw (58), raia wa Ujerumani.

Ushiriki: Ujerumani imeshiriki fainali za kombe la dunia mara kumi na nane (18). Mwaka 1934, 1938, 1954, 1958, 1962, 1966, 1970, 1974, 1978, 1982, 1986, 1990, 1994, 1998, 2002, 2006, 2010 na 2014.

Mafanikio: Kutwaa ubingwa mara nne (1954, 1974, 1990 na 2014).

Kuelekea 2018:

Baada ya kutofanya vizuri kwenye fainali za mataifa ya Ulaya mwaka 2016 zilizofanyika nchini Ufaransa, huku wakiwa wametoka kutwaa ubingwa wa dunia mwaka 2014, kocha Joachim Löw alianza kufanya mabadiliko ya taratibu katika kikosi chake kwa kuwajumuisha wachezaji chipukizi na kuwaondoa baadhi ya wakongwe, ambao wengine walitangulia kutangza kustaafu kuitumikia timu ya taifa.

Akicheza michezo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia kupitia ukanda wa Ulaya (UEFA), kocha huyo alianza kuonyesha matumaini kwa mashabiki wa Ujerumani ambao walikuwa wamevunjwa moyo na matokeo ya fainali za Ulaya za 2016.

Kikosi cha Ujerumani kilipambana bila kuchoka na kufikia lengo la kushinda michezo yote ya kuwania kufuzu na kurejesha matumaini upya ya kutetea ubingwa wa dunia kwa mwaka huu 2018.

Kikosi cha Joachim Löw, hakikuwahi kupoteza mchezo wowote tangu kilipofungwa na Ufaransa kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano ya Ulaya mwaka 2016, jambo ambalo lilidhihirisha ubora wa mabingwa hao wa dunia.

Mwezi uliopita Ujerumani walipoteza kwa mara ya kwanza wakiwa wanacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Brazil kwa kufungwa bao moja kwa sifuri, na juzi walifungwa na Austria mabao mawili kwa moja katika mchezo mwingine wa kirafiki.

Wakiwa katika fainali za kombe la mabara mwaka 2017 zilizofanyika nchini Urusi, Ujerumani walitwaa ubingwa wa michuano hiyo kupitia sera ya kocha Joachim Löw ya kuwatumia vijana kwa asilimia kubwa.

Baadhi ya wachezaji waliounda kikosi kilichoendelea kutisha duniani kupitia michuano ya kombe la mabara ni Jérôme Boateng, Mats Hummels, Manuel Neuer, Toni Kroos, Mesut Özil, Thomas Müller, Mario Götze, Ilkay Gündogan, Marco Reus, Sami Khedira and Leroy Sané.

Baadhi ya wachezaji chipukizi waliokuwepo kikosini wakati wa fainali za kombe la mabara ni Timo Werner, Lars Stindl na Leon Goretzka.

Kutokana na mafanikio hayo kikosi cha Ujerumani chini ya kocha Joachim Löw kinatarajiwa kuendeleza maajabu katika fainali za kombe la dunia za mwaka huu na mashabiki wengine katika mitandao ya kijamii wanaamini taifa hilo lenye watu zaidi ya 82,800,000, litafanikiwa kutetea ubingwa.

Ujerumani wataanza kampeni za kutetea ubingwa huu kwa kucheza dhidi ya Mexico, Uwanja wa Luzhniki mjini Moscow Juni 17, kisha watapambana na Sweden Juni 23, Uwanja wa Fisht Olympic mjini Sochi, na mchezo wao wa mwisho hatua ya makundi watakutana na Korea Kusini Juni 27, Uwanja Kazan mjini Kazan.

Je, Ujerumani itaendeleza ubabe na kurejea tena na kombe nyumbani kwao au itapokonywa? Kaa hapa na Dar24 tukujuze, usipitwe kupitia YouTube Channel yetu ‘Dar24 Media’.

Zaha aeleza sababu ya kwenda Ivory Coast
Arsenal yampigia hesabu Marouane Fellaini

Comments

comments