Ureno ilifuzu Fainali za Kombe la Dunia 2018, kupitia ukanda wa barani Ulaya. Nchi hii ilifanikiwa kuongoza kundi B lililokuwa limesheheni timu za Uswiz, Hungary, Visiwa vya Faroe, Latvia na Andorra.

Ureno ambao ndio mabingwa wa Ulaya, walimaliza michezo ya kuwania kufuzu ya kundi hilo kwa kushika nafasi ya kwanza, na kufikisha alama 27, wakifuatiwa na Uswiz ambao pia walifikisha alama 27.

Ureno walishika nafasi ya kwanza kufuatia kuwa na uwiyano mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa dhidi ya Uswiz.

Jina la utani la timu ya taifa ya Ureno: A Seleção das Quinas (The Navigators).

Mfumo: Kikosi cha Ureno hutumia mfumo wa 4-4-2.

Related imageMchezaji nyota na Nahodha: Cristiano Ronaldo (Real Madrid).

Image result for Bernardo Silva - portugalMchezaji hatari: Bernardo Silva (Manchester City).

Image result for Fernando Santos - portugalKocha: Fernando Santos (63), raia wa Ureno.

 

Ushiriki: Ureno wameshiriki fainali za kombe la dunia mara sita (6). Mwaka 1966, 1986, 2002, 2006, 2010 na 2014. Mwaka huu ni mara ya saba (7).

Mafanikio: Mshindi wa tatu (1966).

 

Kuelekea Urusi 2018:

Kama ilivyo kwa Brazil, Argentina, Hispania na Ujerumani, Ureno ni moja ya timu ambayo inapewa nafasi kubwa kufanya vyema katika fainali za mwaka huu, na wengine wanaamini itatwaa ubingwa, kutokana na kuwa na kikosi bora.

Juhudi na mipango waliokuwa nayo wakati wa fainali za Ulaya mwaka 2016 zilizofanyika Ufaransa, ndizo zinatoa nafasi kwa Ureno kuaminiwa huenda wakaendelea na mwenendo huo, na kufikia malengo ya kufanya vyema.

Ukimtoa Ronaldo ambaye tayari ameshakamata katika vichwa vya mashabiki wengi duniani, wachezaji Bernardo Silva na André Silva wanatajwa kuwa ufunguo wa mafanikio katika fainali za kombe la dunia mwaka 2018.

Hata hivyo, kocha Fernando Santos atakabiliwa na changamoto ya kuwa na safu yake ya ulinzi ambayo ina udhaifu kutokana na mabeki tegemezi kuwa na umri mkubwa, jambo ambalo linleta hofu endapo watakutana na timu yenye safu kali ya ushambuliaji. Pepe ana umri wa miaka 35, José Fonte (34) na Bruno Alves (36).

Ronaldo atahitaji kukiongoza kikosi cha Ureno kama nahodha kwa kufikia mafanikio ya kutwaa ubingwa wa dunia kama ilivyokua wakati wa fainali za Ulaya mwaka 2016.

Pamoja na kutokua na msimu mzuri katika ligi ya Hispania akiwa na klabu ya Real Madrid Ronaldo amefanya vyema kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa kusaidia kuifikissha Real Madrid hatua ya fainali huku akiwa mfungaji bora msimu huu kwa kufunga mabao 15.

Ureno itaanza kampeni za kuusaka ubingwa mwaka huu kwa kucheza dhidi ya Hispania, Uwanja wa Fisht Olympic, mjini Sochi Juni 15, kisha watapambana na Morocco Juni 20, Uwanja wa Luzhniki, mjini Moscow, na mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi watapapatuana na Iran Juni 25, Uwanja Mordovia, mjini Saransk.

Ni Ureno ambayo mwaka huu inaonekana huenda ikawa tishio kubwa kwa mabingwa watetezi, Ujerumani, Brazil yenye hasira za kurejesha heshima yake iliyoyumba kwenye fainali zilizopita, Argentina na miamba mingine.

Endelea kufuatilia mfululizo wa makala hizi tukimulika vikosi vyote vya timu za taifa zinazowania ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka huu nchini Urusi. Tulimaliza kundi A, tuko kundi B. Kesho tutamulika timu nyingine

Dkt. Kimei amwaga chozi hadharani
Gazeti la Mwananchi latakiwa kuomba radhi