Dunia nzima imepata joto la shangwe za mashabiki wa Soka wanaosubiri kushuhudia fainali za Kombe la Dunia, linalofanyika mora moja kila baada ya miaka minne. Mwaka huu mwenyeji wa Mashindano haya ni Urusi, moja kati ya mataifa yenye nguvu kubwa duniani.

Kwa kujali umuhimu wa kombe hili, Dar24 tunakuletea mfululizo wa makala za Kombe la dunia zitakazokusaidia kufahamu kwa ufupi mambo muhimu kuhusu kila kikosi cha timu itakayoshiriki, ili upate picha ya awali ya ‘Nani anaweza kuwa nani’ kwenye fainali hizi. Tukianza na kundi A.

Leo tunakimulika kikosi cha Timu ya Taifa ya Urusi, wenyeji walioko kundi A.

Kundi A (Group A).

Timu za kundi hili ni Urusi, Saudi Arabia, Egypt (Misri) na Uruguay. Leo tunaimulika Urusi.

Urusi (Russia)

Urusi imefuzu moja kwa moja kushiriki fainali za kombe la dunia mwaka huu, kwa tiketi yake ya kuwa mwenyeji wa fainali hizo, ambazo zitafanyika kwa mara ya kwanza nchini kwao tangu zilipoanza mwaka 1930.

Mfumo: Kikosi cha Urusi hutumia mfumo wa 3-5-2.

Image result for Igor AkinfeevMchezaji Nyota: Mlinda mlango wa klabu ya CSKA Moscow, Igor Akinfeev.

Image result for Aleksandr GolovinMchezaji hatari: Aleksandr Golovin kutoka klabu ya CSKA Moscow.

Image result for Stanislav CherchesovKocha: Stanislav Cherchesov (54), raia wa Urusi. Huyu anaweza kuwa na morali ya uzalendo pamoja na jitihada ya kulinda obora wa kazi.

Ushiriki: Urusi wamewahi shiriki fainali za kombe la dunia mara saba (7), tangu kuvunjwa kwa Umoja wa Kisoviet kati ya mwaka 1990 na 1991.

Urusi imeshiriki mwaka 1994, 1998, 2002, 2006, 2006, 2010 na 2014.

Mafanikio: Haikuwahi kuchukua kombe. Mafanikio ya juu zaidi iliyowahi kufikia ni nafasi ya 18 katika fainali za mwaka 1994 zilizofanyika nchini Marekani.

Kuelekea 2018:

Kocha Stanislav Cherchesov, hakufanya vizuri katika fainali za barani Ulaya za 2016 pamoja a kombe la mabara mwaka 2017.

Katika fainali za kombe la dunia mwaka huu anatarajia kumtumia beki chipukizi Viktor Vasin wa klabu ya CSKA Moscow ambaye atashirikiana na  Fedor Kudryashov wa klabu ya Rubin Kazan, Georgi Dzhikiya wa Spartak Moscow.

Mabeki hao watachukua nafasi za wakongwe kama Ignashevich na Vasily Berezutski.

Kocha huyo hupendelea mfumo wa kuwatumia mabeki watatu tofauti na ilivyozoeleka miongoni mwa mashabiki wengi duniani kuona mfumo wa mabeki wanne wakitumika mara kwa mara.

Kikosi cha Urusi kitaongozwa na nyota wake Igor Akinfeev, ambaye ndio gumzo kwa sasa, miongoni mwa mashabiki wa nchi hiyo.

Nyota mwingine ambaye ni gumzo kwa sasa nchini Urusi ni Igor Denisov, ambaye anacheza nafasi ya kiungo mkabaji katika klabu yake ya Dynamo Moscow kwa kusaidiana na Cherchesov.

Washambuliiaji wa Urusi ambao ni hatari kuelekea katika fainali za mwaka huu ni Alan Dzagoev, Fyodor Smolov na Aleksandr Kokorin.

Urusi imepangwa katika kundi la kwanza lenye timu za Saudi Arabia, Egypt (Misri) na Uruguay.

Wenyeji hawa wa mashindano wataanza kampeni za kuusaka ubingwa mwaka huu kwa kucheza dhidi ya Saudi Arabia katika uwanja wa Luzhniki uliopo mjini Moscow Juni 14, kisha watapambana na Egypt mjini Saint Petersburg kwenye uwanja wa Krestovsky Juni 19, na watamaliza michezo ya hatua ya makundi Juni 25 dhidi ya Uruguay, kwenye uwanja wa Cosmos mjini Samara.

Je, Kombe la Dunia litabaki Urusi mwaka huu, au mashabiki wa soka nchini humo watakula kwa macho na kuachwa na kilio?

Usikose kufuatilia uchambuzi mfupi wa timu nyingine inayoshiriki Kombe la Dunia, kesho, hapa hapa Dar24. Toa maoni yako, unadhani nani atanyanya kombe?

Video: Barcelona wawasili Afrika Kusini
Video: Alikiba awataka watanzania wasione haya kuitwa waswahili