Bila shaka unaendelea kufurahia Jumapili tulivu ukitafakari matukio kadhaa ya
michezo nchini, Afrika Mashariki na Duniani kwa ujumla, lakini pia kiu ya
kushuhudia michezo ya Fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi inaongezeka.

Kuiweka sawa kiu hiyo, Dar24 inaendelea kuzimulika timu zinazoshiriki fainali
hizo. Leo tunaendelea na Kundi E tukimulika kikosi cha Timu ya Taifa ya Coasta
Rica, ambacho kimepangwa kwenye kundi hilo pamoja na wababe Brazil, Uswisi
na Serbia.

Timu ya taifa ya Costa Roca inayotegemewa na wananchi zaidi 4,857,274 ilifuzu
fainali za kombe la dunia za mwaka 2018, ikitokea ukanda wa Amerika ya Kati na
Kaskazini Kusini (CONCACAF).

Haikuwa rahisi kwa Costa Rica kufuzu kutokana na kanuni na mlolongo wa
kuwania nafasi kutoka ukanda wa CONCACAF kuwa mrefu.

Costa Roca ilianza kuwania nafasi ya kufuzu katika mzunguuko wa nne kwa
kupangwa kundi B lililokua na timu ya Panama, Haiti na Jamaica.

Ilimaliza michezo ya kundi hilo ikiwa kinara kwa kufikisha alama 16, ikifuatiwa
na Panama alama 10, Haiti alama 4 na Jamaica alama 4.

Baada ya kumaliza katika nafasi ya kwanza Costa Rica ilifuzu kucheza hatua ya
tano ya kufuzu kupitia ukanda wa CONCACAF, ambapo huko ilipangwa katika
kundi moja na timu za mataifa ya Mexico, Panama, Honduras, Marekani (USA)
na; Trinidad & Tobago.

Kanuni za hatua ya tano ambayo ni ya mwisho katika ukanda wa CONCACAF
huzitoa timu tatu kushiriki moja kwa moja fainali za kombe la dunia, ambapo
Costa Rica ilikuwa moja kati ya timu hizo, kufuatia kumaliza katika nafasi ya pili
ikiwa na alama 16, ikitanguliwa na Mexico.

Nafasi ya tatu ilishikwa na Panama kwa alama 13, Honduras nafasi ya nne kwa
kupata alama 13, Marekani walipata alama 12 na kushika nafasi ya tano huku
Trinidad & Tobago waliburuza mkia kwa kukusanya alama 6.

Majina ya utani ya timu ya taifa ya Costa Rica: La Sele (The Selection), La
Muerte (Death), La Tricolor (The Tricolor) na Los Ticos (The Ticos)

Mfumo: Kikosi cha Costa Rica hutumia mfumo wa5-4-1.

Image result for Keylor Navas - costa ricaMchezaji Nyota: Keylor Navas (Real Madrid)

Image result for Marco Ureña - costa ricaMchezaji Hatari: Marco Ureña (San Jose Earthquakes).

Image result for Bryan Jafet Ruiz González - costa ricaNahodha: Bryan Jafet Ruiz González (Sporting CP)

Related imageKocha: Óscar Antonio Ramírez Hernández (53), raia wa Costa Rica.

Ushiriki: Costa Rica imeshiriki fainali za kombe la dunia mara nne (4). Mwaka
1990, 2002, 2006 na 2014.

Mafanikio: Kufika Robo Fainali (2014).

Kuelekea 2018:

Óscar Ramírez amefanikisha ndoto za taifa la Costa Rica kucheza fainali za kombe
la dunia mara mbili mfululizo, baada ya kuchukua nafasi ya Jorge Luis Pinto,
ambaye alilazimika kuvunjiwa mkataba na shirikisho la soka nchini humo, kufuatia
kuwa na mwenendo mbaya wakati wa kuwania kufuzu fainali za mwaka huu.

Ramírez anauamini mfumo wake wa 5-4-1 ambao aliutumia katika michezo ya
kuwania kufuzu na kufanikiwa kuivusha timu yake, hivyo bado anatarajiwa
kuendelea kuutumia wakati wa fainali nchini Urusi.

Kocha huyo ambaye aliwahi kuitumikia timu ya taifa ya Costa Rica kuanzia
mwaka 1985–1997 anajivunia kuwa na wachezaji kama Bryan Ruiz na Celso
Borges.

Ruiz anaiongoza safu ya ushambuliaji ya Costa Rica na Borges huleta muhimili
mzuri katika safu ya kiungo. Malinda mlango namba moja wa Real Madrid Keylor
Navas naye ni tumaini kwa kocha huyo.

Marco Ureña, anaeitumikia klabu ya San Jose Earthquakes katika ligi ya nchini
Marekani anaongeza thamani ya kikosi cha Costa Rica kikiwa kinaelekea kwenye
fainali za kombe la dunia za mwaka huu.

Costa Rica wataanza kampeni za kuusaka ubingwa mwaka huu kwa kucheza dhidi
ya Serbia, Uwanja wa Cosmos, mjini Samara Juni 17, kisha watapambana na
Brazil Juni 22, Uwanja wa Krestovsky mjini Saint Petersburg, na mchezo wao wa

mwisho hatua ya makundi watakutana na Uswiz Juni 27, Uwanja Nizhny
Novgorod mjini Nizhny Novgorod.

Kuwa na Jumapili njema, endelea kuifuatilia kwa karibu Dar24 kwenye tovuti,
mitanado ya kijamii na YouTube ambayo ni Dar24 Media ili uwe karibu na Urusi
mwaka huu.

Kesho tutalifunga kundi E na kuanza kundi lingine hadi tujue nani amekuwa nani
na amejipanga vipi.

 

Magazeti ya Tanzania leo Juni 4, 2018
Museveni ashinikiza Kanisa kumtangaza Nyerere Mtakatifu