Urusi imeitaka Marekani kusubiri matokeo ya athari za mashambulio yake iliyoyafanya nchini Syria kwa kushirikiana na washirika wake.

Urusi imeyasema hayo kupitia kwa balozi wake nchini Marekani, Anatoly Antononov ambapo ameitaka Marekani itarajie majibu ya shambulio hilo.

Kwa upande wake, Rais wa Syria, Bashar al-Asaad amesema kuwa mashambulio yaliotekelezwa na Marekani, Uingereza na Ufaransa yamemfanya kuwa jasiri zaidi ya alivyokuwa hapo awali kukabiliana na wapinzani wake.

Mapema rais Trump alisema kuwa mashambulio hayo yalikuwa yakilenga viwanda vya kutengeneza silaha za kemikali zinazolaumiwa kwa kutumika katika shambulio kwa raia wanaoishi mjini Douma wiki moja iliyopita.

Hata hivyo, Trump amesema kuwa Marekani na washirika wake wametumia uwezo wao kupambana dhidi ya ubepari na ukatili, huku akiitupia lawama Urusi kwa kushindwa kukabiliana na silaha za kemikali nchini Syria.

Mapadre 3 wafariki dunia ndani ya saa 72
Merkel aunga mkono mashambulizi ya kijeshi nchini Syria