Rais wa Urusi, Vladimir Putin ameongeza nguvu zaidi ya kulishambulia kundi la ISIS nchini Syria ambapo jana ilishusha mabomu mazito ambayo yanadaiwa kuwa hayajawahi kupigwa duniani kote kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita.

Putin alitangaza vita dhidi ya magaidi na kueleza kuwa atawatafuta magaidi walioidondosha ndege ya nchi yake na kusababisha vifo vya watu 224 katika eneo la Mlima Sinai. Ingawa kundi la ISIS halikusema chochote kuhusu tukio hilo, inasadikika kuwa kundi hilo huenda likawa limehusika.

Vikosi vya Urusi na Ufaransa vimefanya mashambulizi makali ya ndege na kushusha mabomu mazito katika maeneo ambayo Rais wa Marekani, Barack Obama alikuwa hajaruhusu majeshi yake kushambulia kwa kuhofia madhara.

Jeshi la Ufaransa limeeleza kuwa ndege za kivita za Ufaransa na Urusi zimeshambulia vikali makao makuu ya Kundi la Islamic State ya Raqqa nchini Syria yanayofahamika kama ‘Caliphate’ ambako.

Hatua hizo za kijeshi dhidi ya IS zinakuja  baada ya kundi hilo kushambulia Ufaransa na kutekeleza tukio la kigaidi lililochukua uhai wa watu 129 huku 135 wakijeruhiwa.

Kafulila Atinga Rasmi Mahakama Kuu
Video: Angalia Algeria Ilivyoituliza Taifa Stars Jana