Urusi imesema kuwa imefanikiwa kufanya jaribio la kombora lisiloweza kuzuilika ambalo ni miongoni mwa makombora yaliyotangazwa na Rais wa nchi hiyo, Vladmir Putin katika kampeni zake.

Wizara wa ulinzi ya Urusi imeonyesha video ambayo ilikuwa ikionyesha kombora hilo likifyatuliwa kutoka kwenye ndege ya kivita.

Aidha, Kombora la Kinzhal limeelezwa kuwa linaweza kusafiri mara kumi zaidi ya makombora mengine ambapo haliwezi kuonekana katika rada za kijeshi.

Hata hivyo, hatua hiyo ya jaribio la silaha hiyo ya nyuklia imefanyika ikiwa ni utekelezaji wa sera ya rais wa nchi hiyo, Vladimir Putin ambaye anatarajiwa kuchaguliwa tena kuendelea kuiongoza nchi hiyo hivi karibuni.

 

Azam FC yawashusha mabingwa watetezi
Video: Tundu Lissu operesheni ya 18, Mwigulu awageuzia kibao wapinzani