Mamlaka za Serikali nchini Ukraine, zimesema mashambulizi ya makombora ya Urusi yameathiri karibu nusu ya mifumo yake ya nishati, huku viongozi katika mji mkuu wa Kyiv wakionya kwamba jiji hilo linaweza kukabiliwa na kuzimwa kabisa kwa gridi ya umeme wakati huu wa msimu wa baridi.

Katika miezi tisa ya vita, Urusi imeendesha baadhi ya mashambulizi makubwa zaidi nchini Ukraine na kuilenga miundombinu ya kiraia.

Maafisa wa Ukraine wanasema, Urusi imeharibu nusu ya mifumo ya mitambo ya nishati na joto nchini humo huku hali ya hewa ikizidi kuwa ya baridi. Picha ya Vyacheslav Madiyevskyy/ Reuters.

Rais wa Ukraine, Volodymyrr Zelensky kupitia hotuba yake jana usiku (Novemba 18, 2022), amesema kuwa karibu watu milioni 10 hawana umeme nchini humo.

Umoja wa Mataifa UN, umesema uhaba wa umeme na maji nchini Ukraine unatishia kutokea kwa maafa makubwa ya kibinadamu katika msimu huu wa baridi na hivyo kuona ipo haja ya kutafuta namna zaidi ya kupambania hatua stahiki kuikabili hali hiyo.

Sony Music wamuibua Aslay mafichoni
Tangazo la Serikali lasababisha mauaji Gerezani