Mwenyeji wa Kombe la mabara nchi ya Urusi imeanza vizuri mashindano hayo mara baada ya kuishushia kipigo New Zealand cha mabao 2-0.

Magoli ya Urusi yalipachikwa kimiani na mchezaji wa New Zealand, Michael Boxal katika dakika ya 31 mara baada ya kujifunga huku jingine likifungwa na mshambuliaji wa timu ya Urusi, Fyodor Smolov dakikia ya 69 kipindi cha pili.

Timu  zote zilisimama uwanjani wakisikiliza hotuba iliyotolewa na rais wa Urusi, Vladimir Putin  na  rais  wa  shirikisho  na  kandanda duniani (FIFA), Gian Infantino kabla ya kuruhusiwa kukamilisha maandalizi  ya  pambano  hilo.

Hata hivyo, kabla ya kuanza kwa michuano hiyo, Putin aliwataka wachezaji wa timu hiyo kupata matokeo mazuri ili kuweza kuwafurahisha wananchi wa Urusi

 

Video: Jinsi Mwakyembe alivyomjibu Kubenea
Meli ya kijeshi ya Marekani yapata ajali baharini

Comments

comments