Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, Vassily Nebenzia, ameonya kuwa shambulio lolote la anga litakalofanywa na Marekani nchini Syria litasabaisha kulipuka kwa vita baina ya Moscow na Washington na kuongeza kuwa Urusi haiwezi kuepuka uwezekano wowote wa kutokea vita baina ya mataifa hayo.

Nebenzia ameituhumu Marekani na washirika wake kwa kuiweka amani ya mataifa katika hali hatari zaidi kwa kile alichokiita sera za ukatili na kusema kuwa hali ilivyo kwasasa ni hatari kupita kiasi.

Aidha, Rais wa Marekani, Donald Trump anatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi wa mataifa ya Ufaransa na Uingereza kujadili juu ya kutoa kauli ya pamoja kwa kile wanachoamini kuwa matumizi ya sialaha za kemikali yaliyofanywa na Syria kwenye maeneo ya kitalii yanayoshikiliwa na waasi.

Hata hivyo, Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza imesema kuwa baraza la mawaziri limekubaliana kuwa matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria hayakubaliki.

 

Mhagama awataka viongozi wa dini kuliombea taifa
Video: Sakata la Makonda laanza kuzaa matunda, mmoja akamatwa

Comments

comments