Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov amesema kuwa ripoti kuhusu shambulio la silaha za kemikali ni njama za Marekani kutaka kuichafua nchi hiyo.

Marekani, Ungereza na Ufaransa zimesema kuwa zina ushahidi wa kutosha, hivyo wanajiandaa kufanya mashambulizi ya kijeshi nchini Syria.

Aidha, Urusi na mshirika wake Syria, imeitahadharisha Marekani kuwa mashambulizi ya anga yanaweza kusababisha vita mpya.

Wataalam wa masuala ya silaha za kemikali wako njiani kuelekea Ghouta kutafuta ushahidi, wa kile kinachodaiwa kuwa silaha za kemikali zilitumika kufanya mashambulizi mwishoni mwa wiki iliyopita.

Hata hivyo, Serikali ya Rais wa Syria, Bashar Al Assad ambayo inaungwa mkono na Urusi imekana kuhusika na shambulio lolote la kemikali, ikisema ripoti hizo ni za kutunga.

Uganda yakubali kuwapokea wakimbizi kutoka Israel
Makonda afanikisha watoto 205 kuhudumiwa na baba zao

Comments

comments