Kitengo cha ulinzi na usalama cha Urusi (FSB) kimeeleza kuwa kimemkamata raia wa Marekani aliyekuwa anafanya kazi ya upelelezi jijini Moscow.

Idara hiyo imemtaja Mmarekani huyo kwa jina la Paul Whelan ikieleza kuwa alitiwa mbaroni Desemba 28 mwaka huu baada ya kumfuatilia kwa muda mrefu.

Endapo atakutwa na hatia, atakabiliwa na kifungo cha kati ya miaka 10 na 20 jela, kwa mujibu wa chombo cha habari cha Urusi kinachoitwa Tass.

Tuhuma za kuwakamata wapelelezi wa Marekani na Uingereza zimekuwa zikitajwa na Urusi mara kadhaa. Vivyo hivyo kwa Marekani.

Mapema mwezi huu, Urusi ilimshtaki Mmarekani, Maria Butina ambaye alikutwa na hatia ya kufanya kazi za kisiasa kwa niaba ya Marekani nchini humo.

Mwezi Machi mwaka huu, Uingereza na baadhi ya nchi washirika ziliwafukuza wanadiplomasia 100 wa Urusi kufuatia tukio la aliyekuwa mpelelezi wa Urusi, Sergei Skripal na binti yake kupewa sumu na watu wasiojulikana.

Uingereza ilisema kuwa inaamini Urusi ndiyo iliyotekeleza kitendo hicho kutokana na kumtaja Skripal kama msaliti.

Mayweather ampiga kikatili Mjapan Nasukawa
Makala: Wateule watano wa JPM ‘waliokiki’ zaidi 2018 na mambo yao