Urusi imesema leo kuwa “kampeni ya habari za uwongo” kuhusu madai ya kuwekewa sumu kiongozi wa upinzani Alexei Navalny inatumika kushinikiza vikwazo vipya dhidi ya nchi hiyo.

Serikali ya Urusi imetoa taarifa baada ya mawaziri wa mambo ya kigeni wa Kundi la G7 kuitaka Urusi kuwatafuta haraka na kuwashitaki waliohusika na tukio hilo la Navalny kudaiwa kupewa sumu aina ya Novichok inayoathiri mishipa ya fahamu.

Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Urusi imesema kampeni hiyo ya habari za uwongo haihusu afya ya Navalny wala kutafuta sababu halali za kulazwa kwake.

Katika taarifa yake ya kulijibu kundi la G7, Urusi pia imesisitiza tuhuma kuwa Ujerumani, ambako Navalny alihamishiwa, imekuwa ikikataa kuishirikisha Urusi katika uchunguzi wake kuhusu kisa hicho.

Sven Vandenbroeck aahidi mabadiliko dhidi ya Mtibwa Sugar
Zlatko Krmpotic: Kikosi kitaimarika