Rais wa Urusi, Vladimir Putin amepiga marufuku safari ya ndege zote za Urusi kuelekea nchini Misri hadi pale itakapobainishwa kwa usahihi sababu zilizopelekea kuangushwa kwa ndege ya nchi hiyo, Metrojet Flight 9268 katika eneo la Sinai, Jumamosi iliyopita.

Ndege Urusi

Uamuzi huo wa Rais Putin umekuja kufuatia mapendekezo yaliyotolewa na mkuu wa kitengo cha huduma za ulinzi za Urusi, Alexander Bortinikov kupitia kikao cha kamati maalum iliyoundwa kuchunguza chanzo cha kuanguka kwa ndege hiyo, kikao kilichorushwa moja kwa moja na Televisheni ya Taifa ya nchi hiyo.

Urusi imepinga vikali ripoti ya uchunguzi uliofanywa na Marekani na Uingereza iliyodai kuwa huenda ndege hiyo ilianguka baada kufuatia kulipuka kwa bomu lilipandishwa kwenye ndege hiyo na mmoja kati ya wafanyakazi wa ndege hiyo. Ripoti hiyo imeeleza kuwa shambulio hilo linaweza kuwa la kigaidi kama sehemu ya kupinga uamuzi wa Urusi kuingiza vikosi vyake nchini Syria kupambana na kundi la ISIS.

Hata hivyo, ripoti hiyo pia ilipingwa vikali na viongozi wa serikali ya Misri.

Mahakama Yazima Neema Ya Nyongeza ya Mishahara ya Walimu Kenya
Muonekano Wa Mkapa Ulivyosawazisha Mambo