Kocha Mkuu wa US Monastir ya Tunisia, Novic Darko, ameshindwa kujizuia na kutamka kuwa kama akipewa nafasi ya kusajili Mshambuliaji msimu ujao, basi chaguo lake la kwanza litakuw ana Fiston Mayele.

Kocha Darko alitoa kauli hiyo mara ya baada ya kikosi chake kukubali kichapo cha 2-0 kutoka kwa Young Africans juzi Jumapili (Machi 19) katika mchezo wa Kundi D la Kombe la Shirikisho Barani Afrika, Uwanja wa Mkapa, Dar es salaam.

Darko amesema kwa muda mrefu anamfuatilia Mayele na amekiri ni mshambuliaji anayejua kufunga.

Kocha huyo kutoka Ulaya ya Mashariki amesema Mayele ni aina ya washambuliaji anaotamani kufanyakazi nao huku akiamini siku moja atafanikiwa kuwa naye.

Ameongeza kuwa, anaamini kama mshambuliaji huyo akiendelea kujituma zaidi, atafika mbali kutokana na kiwango kikubwa alichonacho cha kufunga na kutengeneza mabao.

“Wachezaji wengi walikuwa tishio katika mchezo huu tuliocheza dhidi ya Young Africans, lakini Mayele ndiye alikuwa tisho kubwa, kwani aliweza kuisumua safu yangu ya ulinzi.”

“Ni mchezaji ninayetamani kufanya naye kazi, kama ikitokea nikihitaji mshambuliaji katika kikosi changu msimu.” Amesema Darko

Mayele aliifungia Young Africans bao la pili akitanguliwa na Kennedy Musonga aliyeitanguliza timu hiyo kuizamisha US Monastir ugenini Dar es salaam.

Rais US Monastir aivulia kofia Young Africans
Baleke: Mashabiki wa Simba wataendelea kufurahi