Klabu ya Simba SC imedai inawaweza kuwasafirisha wachezaji wake 4 Kati ya 5 kwa usafiri binafsi (Private Car) ambao wako nje ya nchi kutokana na mipaka ya nchi yao kufungwa, huku kukiwa hakuna ndege zinazoingia wala kutoka kwenye nchi hizo kutokana na janga la Corona.

Uongozi wa Simba umedai iwapo hali itakuwa nzuri na watakuwa na uhakika wa ligi kurejea hivi karibuni na bado ya mipaka ya nchi ambazo wanatoka wachezaji wao imefungwa, watatumia njia mbadala kuwarejesha nchini kwa ajili ya ligi kuu Tanzania.

Wachezaji wa Simba ambao wapo nje ni Francis Kahata (Kenya), Meddie Kagere (Rwanda), Luis Miquisson (Msumbuji), Clatous Chama (Zambia) na Sharaf Shiboub (Sudan). Ni mchezaji mmoja tu (Shiboub) ambaye hayupo mpakani mwa Tanzania ambaye anaweza akashidwa kurejea.

Machi 17, mwaka huu TFF ilisimamisha ligi zake zote ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufuatia mlipuko wa virusi vya ugonjwa wa corona duniani kote.

Ligi Kuu ilisimama huku Simba SC ikiwa inaongoza kwa pointi zake 71, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 54 baada ya timu zote kucheza mechi 28, wakati vigogo, Yanga SC ni wa tatu kwa pointi zao 51 za mechi 27 na Namungo wa nne wakiwa na pointi 50 za mechi 28.

Hali ni mbaya kwa Singida United inayoshika mkia kwa pointi zake 15 za mechi 29, nyuma ya Mbao FC pointi 22 mechi 28, Alliance FC pointi 29, mechi 29, Mbeya City pointi 30 mechi 29 na Ndanda FC pointi 31 mechi 29.

Wolper: Siwezi kumpa Sumu Harmonize, Sara nimfundishe kuishi naye
CoronaTanzania: Mgonjwa wa tatu amepona, hakuna kisa kipya