Julai 27 mwaka huu itakua siku rasmi ya kufunguliwa kwa dirisha kubwa la usajili kwa England na kuhitimishwa Oktoba 05.

Taarifa iliyotolewa na EPL imeeleza kuwa dirisha la usajili wa wachezaji wa ndani litaendelea hadi oktoba 16 kwa klabu za madaraja yote nchini England.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, kwa sasa klabu yoyote haitaruhusiwa kufanya usajili wa mchezaji yoyote, hadi tarehe tajwa itakapofika ili kuwawezesha wachezaji kutulizana kwenye sehemu zao za kazi, hadi mwishoni mwa msimu huu 2019/20.

“Hakuna usajili wowote ambao unaweza kufanyika katika kipindi hiki hadi tarehe tajwa ndio tunaweza kuanza.” Imeeleza taarifa ya EPL.

Hata hivyo EPL haijatanga tarehe rasmi ya kuanza msimu mpya wa ligi, licha ya baadhi ya vyombo vya habari nchini England kuripoti kuwa, huenda msimu wa 2020-21 ukaanza Septemba 12.

Msimu huu 2019/20 umebakisha michezo miwili kwa kila timu shiriki, huku Liverpool wakitawazwa kuwa mabingwa.

Zidane aipa Real Madrid taji la 34
Jose Mourinho awatosa Man Utd, ataja 11 bora

Comments

comments