Vigogo wa soka wa Cataluña-Hispania FC Barcelona, wanajihami kumsajili beki wa Manchester City Eric Garcia kwa ada ya Euro milioni 27.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 19, amekua akipewa nafasi ya kucheza mara kwa mara na meneja wa Manchester City Pep Guardiola, na ameonyesha kuwa na uwezo mkubwa kisoka, lakini mpaka sasa amegoma kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia matajiri hao wa mjini Manchester.

Maamuzi ya kugoma kusiani kandarasi mpya, yameifanya klabu ya FC Barcelona kuhitaji kumrejesha nyumbani kinda huyo, lakini ada ya kumng’oa Etihad Stadium imekua ukakasi kwao.

Wakati klabu ya Manchester City wakitajwa kuwa wanahitaji Euro milioni 27, kumuachia nyota huyu FC Barcelona wanasema wapo tayari kulipa nusu ya gharama hiyo iliyotajwa (Euro milioni 15).

Guardiola aameshathibitisha kuwa staa huyu anataka kuondoka klabuni hapo, lakini uongozi wa Man City unahitaji kuepuka kumuachia aondoke kama mchezaji huru msimu ujao, hivyo watahitaji kutazama tena mpango wao.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Agosti 12, 2020
Kampuni ya Coca-Cola yaisaini dili Ufaransa, Uholanzi