Mabingwa wa soka nchini England (Chelsea), wanatarajia kupata sehemu ya mgao wa fedha za usajili wa mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Misri Mohamed Salah, ambaye anakaribia kutua Liverpool akitokea AS Roma ya Italia.

Liverpool wanatarajia kulipa Pauni milioni 40 kama ada ya uhamisho wa usajili wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ambayo itaweka rekodi ya usajili uliowagharimu kiasi kikubwa cha pesa katika historia ya klabu hiyo ya Merseyside.

Chelsea watanufaika na mgao wa fedha zitakazolipwa kwenye klabu ya AS Roma, kutokana na mkataba wa makubaliano walioingia na wababe hao wa Stadio Olimpico wakati wakimsajili Salah mwaka 2016.

Salah alijiunga na AS Roma kwa Pauni milioni 12, baada ya kumaliza zoezi la kuitumikia klabu hiyo kwa mkopo, na makuibaliano yaliyoafikiwa na pande hizo mbili ni kulipwa kwa asilimia 10 ya ada yake ya uhsamisho endapo ataihama The La Maggica.

Kwa hesabu hizo, Chelsea watapata mgao wa Pauni milioni nne, endapo Liverpool wataafiki kutoa ada ya usajili ya Pauni milioni 40, kwa ajili ya uhamisho wa mshambuliaji huyo kutoka nchini Misri.

Msimu uliopita Salah alifunga mabao 15 na kusaidia mafanikio ya AS Roma iliyomaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ya Italia Serie A.

Juhudi hizo zimemvutia meneja wa Liverpool Jurgen Klopp, kutamani kufanya kazi na Salah, kama mbadala wa mshambuliaji kutoka nchini Senegal Sadio Mane, ambaye alikosa sehemu ya mwisho ya msimu wa 2016/17.

Young Africans Wanawa Kwa Haruna Niyonzima
Marekani yaendeleza ubabe Syria, yaitungua ndege nyingine