Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na TAMISEMI, Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za Serikali za Mitaa zinaendelea na usajili wa wakulima kwenye mfumo wa M-Kilimo ili waweze kutambuliwa, kutoa huduma kwa njia ya simu na pia Serikali kutoa huduma zingine kwa urahisi.

Aidha mpaka sasa Mikoa 13 imewasajili wakulima na imeweza kufikia asilimia 50 ya kwenye mfumo huo wa M-Kilimo

Akizungumzia hali ya usajili wa wakulima mpaka hivi sasa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Profesa Siza Tumbo, amesema kuwa Mikoa 12 bado ipo chini ya asilimia 50 Kwenye usajili wa wakulima.

Naibu katibu Profesa Tumbo, ameeleza kuwa Mikoa minne (4) ambayo ni Njombe, Arusha, Simiyu na Singida imeweza kufikia lengo la asilimia 100 na zaidi.

Amesema kuwa Mikoa ya Shinyanga, Kagera na Dar-es-Salaam bado wapo chini ya asilimia 30, hivyo kuwasihi kuongeza kasi ili kufikia malengo ya Serikali.

Sambamba na hayo yote Wizara ya Kilimo inatoa shukrani za dhati kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya/Halmashauri, Watendaji Wakuu na ngazi ya Mikoa na Maafisa Kilimo na Wagani wote kwa kazi kubwa ya kuwezesha, kuhamasisha na kusajili wakulima kwenye mfumo wa M-Kilimo.

Manara afunguka uwekezaji wa Bilioni 20 Simba SC
Orodha ya vituo vitakavyotoa chanjo ya uviko 19 Nchini