Mwimbaji wa RnB, Usher Raymond anakumbwa na kesi ya madai ya dola za kimarekani milioni 10 kwa tuhuma za kumuambukiza mwanamke mmoja ugonjwa wa zinaa.

Mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina la Jane Doe amefungua kesi hiyo ya madai akidai kuwa alifanya mapenzi na mkali huyo wa ‘Love in This Club’ mara mbili mwaka huu, April 16 na Aprili 28.

Doe anadai kuwa Usher alishiriki naye ngono kwa mara ya kwanza kwa kutumia kondomu lakini mara ya pili wawili hao waliweka kondomu pembeni na kwamba muimbaji huyo alifanya makusudi huku akijua alikuwa na maradhi ya zinaa.

Alisema alibaini hayo baada ya kugundua kuwa kuna mwanamke aliyeambukizwa ugonjwa huo na Usher mwaka 2012, lakini Usher hakumueleza hilo ili achukue tahadhari.

Kupitia nyaraka alizowasilisha mahakamani, mwanamke huyo amedai kuwa Usher alifanya uzembe au makusudi huku akiijua hali yake kiafya. Hata hivyo, hakuweka wazi kama vipimo vya kitabibu vilionesha ameambukizwa ugonjwa huo.

Usher ameingia kwenye mtego huo wa tuhuma nzito za kuchepuka na kutaka kuambukiza ugonjwa wa zinaa ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipofunga ndoa na Grace Miguel, Septemba mwaka 2015.

Kwa upande mwingine, Tameka ambaye ni mke wa zamani wa Usher waliyetalakiana mwaka 2009 amesema kuwa afya yake iko vizuri na kwamba suala hilo la magonjwa ya zinaa halikuwa tatizo kwake na sio tatizo linalomhusu sasa.

Marekani yaridhia kuiwekea vikwazo Urusi
Rais Magufuli: Aliyemuita Kafulila tumbili yeye ndiye tumbili kwa IPTL