Usher Raymond leo ameachia albam yake mpya aliyoibatiza jina la ‘A’, saa chache baada ya kutangaza ujio huo.

Albam hii ambayo ni kazi ya kwanza kutoka kwa Usher ndani ya kipindi cha miaka miwili, imempa shavu zito mkali wa trap, Zaytoven.

Wengine walioshirikishwa kwenye albam hii ni pamoja na Future kwenye ngoma ‘Stay at Home’ na Gunna kwenye ‘Gift Shop’.

Ameisindikiza albam yake na kionjo cha video kilichochukuliwa katika maeneo mbalimbali.

Isikilize A yenye ngoma nane hapa.

Video: Zaiid akumbushia Gigy Money alivyomchongea BASATA
Kanye west asifu kofia ya Rais Trump

Comments

comments