Tanzania imekuwa kivutio kikubwa cha watalii kutoka mataifa mbalimbali hususani maeneo ya Serengeti National Park na Mlima Kilimanjaro.

Msanii maarufu wa Marekani Usher Raymond pamoja na familia yake wapo ziarani nchini Tanzania, na leo wametembelea eneo la hifadhi ya wanyama pori la Serengeti National Park.

 Raymond kupitia ukarasa wake wa twitter ameweka picha ikionesha yupo katika hifadhi hiyo wakifurahia mazingira yeye na familia yake.

 “So amazing to experience this beauty with my family” ameandika Usher Raymond kwenye kurasa wake wa twitter wakati akiwa katika hifadhi ya taifa ya Serengeti.

Usher Raymond

Usher Raymond akipiga picha na familia yake katika mbuga ya Serengheti nchini Tanzania

Gerard Pique atamba kutwaa ubingwa wa Hispania, Ulaya
Juventus Yaendelea Kujiimarisha, Yamuita Costa