Dakika chache baada bondia wa Australia, Jeff Horn kutangazwa mshindi dhidi ya Pacquiao katika pambano lililofanyika mapema leo, umegeuka gumzo kwenye vyombo vya habari na mitandaoni, ukipingwa vikali.

Tarakimu za mahesabu ya kielekrtoni zilizotolewa na Top Rank ni sehemu ya chanzo cha gumzo hilo zito, zikionesha ushindi wa wazi kwa Pacquio kwa asilimia nyingi kwenye kila sekta dhidi ya Horn.

Kwa mujibu wa takrimu hizo, Pacquiao anaonekana kuwa alifikisha ngumi za wazi 182 dhidi ya 92 tu za Horn. Pia, inaonesha Pacquiao akiwa na asilimia 32 ya makombora yake dhidi ya asilimia 15 tu za Horn.


Baadhi ya watangazaji wa vyombo vya habari waliokuwa uwanjani hapo wakishuhudia pambano hilo pia walishindwa kuvumilia na kueleza kuwa matokeo yaliyotangazwa ni ya ajabu katika historia ya masumbwi.


Wengi wanaikumbushia kauli ya muamuzi wa pambano hilo katika raundi ya 9 akitishia kumaliza pambano endapo Horn hatajitutumua zaidi kwenye raundi ya 10.

Pia, wakosoaji wa pambano hilo wanadai kuwa Horn alionesha jitihada nyingi lakini hali yake ilikuwa mbaya kwa kusambaratishwa sura yake wakilinganisha na Pacquiao.

 

Horn, alipambana akiwa nyumbani kwao Australia mbele ya umati wa watu zaidi ya 55,000 waliohudhuria. Ushindi wake ni heshima kubwa kwa nchi hiyo.

?Live: Majadiliano ya Kamati ya bunge kuhusu marekebisho ya sheria ya Madini
CCM yajipanga kuyarudisha majimbo yake