Idadi ya nchi za Afrika
Bara la Afrika lina nchi 54 ambazo zinatambulika na Umoja wa Mataifa.

Namna timu tano (5) zinavyofuzu kushiriki Kombe la DUNIA Nchini Qatar, 2022.

Katika bara la Afrika kuna hatua tatu (3) Ili kufikia kupata timu tano (5) zitakazo wakilisha Bara la Afrika kwenye Kombe la Dunia.Hatua ya Awali ya mtoano.

Hatua ya Awali ya mtoano

Utaratibu uliowekwa na Shirikisho la Afrika CAF, ni kwamba, katika timu 54, kuna timu 28 ambazo zinashiriki hatua ya Awali ya mtoano. Timu hizi zinapatikana kwa utaratibu ufuatao.

Timu 26 ambazo ziko Juu katika Msimamo wa FIFA (FIFA ranking) hazishiriki kwenye hatua ya mtoano, na timu 28 za chini ndo zinacheza mtoano kwa kupangwa makundi 14 na kila timu inacheza na mwenzake mechi mbili, nyumbani na ugenini.

Ambazo washindi katika Michezo hiyo miwili, wanakwenda kuungana na timu 26 za Juu na kuzaa timu 40.

Tanzania iko katika Kundi la Timu 28 za katika Msimamo wa FIFA (FIFA ranking) ambapo Tanzania katika hatua hii ilipangwa na Burundi ambapo katika Michezo miwili, kule Burundi, TANZANIA ilitoka sare ya Moja kwa Moja. Na mchezo wa pili uliochezwa Dasalamu, katika dakika 90, za awali ngoma ilikuwa moja kwa Moja. Zikaongezwa dakika 30, bado Matokeo hayakubadilika, ndipo tukaenda kwenye matuta na Tanzania tulishinda 3 kwa 0, golini akiwa Juma Kaseja.

Hatua ya pili makundi

Baada ya timu 14 kupatikana Kutoka kwenye mtoano, na kuungana na timu 26, hizo jumla ya timu 40, yanatengenezwa makundi 10 kila Kundi likiwa na timu 4.

Katika kila Kundi, kila timu itacheza na timu nyingine nyumbani na ugenini, ambapo anayeongoza Kundi kwa kila Kundi anapita. Ambapo zitapatikana timu 10. Kutoka makundi kumi (10)

Hatua ya tatu, mtoano

Katika hatua hii, timu 10 zilizoongoza makundi, zinacheza mtoano, na namna inavyopangwa ni kwamba timu tano za Juu katika Msimamo wa FIFA (FIFA ranking) zinacheza dhidi ya timu tano za chini.

Wanacheza Michezo miwili nyumbani na ugenini. Washindi katika mtoano huu ndo wanashiriki ama wanawakilisha Bara la Afrika katika Kombe la DUNIA la FIFA huko nchini Qatar, mwaka 2022.

Kama Tanzania tutaongoza Kundi, Basi tutacheza mtoano na timu Moja wapo iliyojuu katika Msimamo wa FIFA au tutacheza na timu iliyochini ya msimamo wa FIFA.

Timu 10 za Afrika zinazokwenda kushindana kupata 5 za kwenda kombe la Dunia Qatar 2022 Kwa msimamo wa sasa ni Algeria, Tunisia, Misri, Nigeria, Senegal, Mali, Afrika Kusini, Tanzania, Morocco na Ivory Coast

Imeandaliwa na Chicharito Anderson

Natumbua bila kuangalia kabila- Rais Samia
Kichapo chamharibu Deontay Wilder