Mshahara ni pesa ambayo mtu hulipwa baada ya kukamilisha kazi fulani, kila mfanyakazi ana mshahara wake kulingana na kazi aliyofanaya na makubaliano aliyoingia na bosi wake, wapo wanaolipwa kwa dakika, saa, siku, wiki, mpaka kwa mwezi.

Wengi wao mishahara yao haijawahi kutosha kutokana na majukumu mengi  na matumizi ambayo siyo ya lazima ambayo watu hufanya bila kuzingatia kesho yao na ndio maana wafanyakazi wengi huishiwa mishahara kabla ya mwezi kuisha.

Waswahili wanasema hela ya mshahara huwa haitoshi, si kweli kwani inategemea na matumizi ya mtu.

Je, ni vitu gani unavipa kipaumbele na hela yako?, ukilipwa laki moja kesho ukalipwa laki tano bado kama haujanga vizuri matumizi yako utaona hiyo pesa haitoshi.

Hivyo tazama mambo ambayo haupaswi kuyafanya katika mshahara wako.

  1. Ukilipwa pesa yako usitumie simu kutangaza kuwa una pesa, kwa kufanya hivyo utapokea simu nyingi zenye ushawishi tofauti wengine watataka wakukope, wengine watataka mkafanye starehe ya kunywa na wengine watakuletea shida zao wakiomba uwasaidie wakiamini una pesa hivyo kamwe usipige picha na kurusha mtandaoni kujionesha una hela.
  2. Ukilipwa mshahara usitumie pesa yote kuwekeza katika biashara fulani kwa kuona mtu fulani amefanikiwa kupitia biashara hiyo, katika biashara kuna mawili kupata au kukosa hivyo anza kidogo endapo unawazo la kuwekeza tumia sehemu ndogo ya mshahara wako kuwekeza ili ikizaa matunda uweze kufanya kitu kikubwa.
  3. Usitumie pesa yako kufanya matumizi ambayo sio ya ulazima katika maisha yako, jitahidi kutumia pesa yako katika mambo ya msingi ili uweze kuhifadhi kiasi cha fedha unachokipata.
  4. Usitamani kununua vitu ambavyo huwezi kugharamia, hii itakufanya utumie pesa yako vibaya na kufanya pesa yako ikae kwa muda mfupi.

 

Wafahamu watu 10 wenye ushawishi mkubwa zaidi Duniani
Mwanasheria ang'aka tuhuma za ubakaji dhidi ya Chris Brown

Comments

comments