Kwa waliosoma vitabu vya dini wanaelewa kuwa maji yalikuwa muhimu sana kwenye uso wa dunia na kwamba kabla hatujawa na dunia hii tuliyonayo, maji yalikuwapo na yalikuwa yametanda kila sehemu.

Kama ilivyokuwa umuhimu wa maji hayo hata kabla ya kuwepo dunia, maji haya yaligeuzwa kuwa muhimu sana kwenye miili yetu na uhai wetu unategemea uwepo wa maji haya.

Maji huchukua asilimia takribani 75 ya mwili wote wa binadamu. Lakini kwa bahati mbaya watu wengi wamekuwa wakifikiria zaidi kuhusu chakula kuliko maji. Haya ni baadhi ya maajabu ya maji ambayo maji yataufanyia mwili wako:

1. Usipokunyuwa maji utakufa haraka

Kwa ufupi, ni dhahiri kuwa usipokunywa maji utakufa. Maji ni muhimu zaidi kwenye mwili wa binadamu hata kuliko chakula. Ni dhahiri kwamba sipokula chakula utakufa, lakini utakufa ndani ya siku chache zaidi kama hautakunywa maji.

2. Huzuia Saratani

Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa watu wenye tabia za kunywa maji mengi kadri inavyotakiwa (angalau lita 3 kwa siku) wana nafasi nzuri zaidi ya kupunguza uwezekano wa kupata saratani kwa asilimia 45.

3.  Hupunguza msongo wa mawazo

Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa ukosefu wa maji ya kutosha mwilini kunaweza kuathiri uwezo wa kufikiria wa binadamu na kumfanya aweze kuchanganyikiwa na mambo kwa uharaka zaidi kuliko mtu ambaye anakunywa maji mengi. Mtu anayekunjwa maji mengi huwa na uwezo mzuri wa kufikiria kwa utulivu na kuikaribisha furaha zaidi.

Maji

Ukiwa na msongo wa mawazo, utakuwa katika wakati mgumu zaidi endapo utakuwa haunywi maji mengi kwa kuwa uwezo wako wa kufikiria umeathiriwa na ukosefu wa maji.

4. Huongeza uwezo wa kufanya kazi

Mwili wa binadamu ni kama mashine inayofanya kazi kwa kutumia mfumo wa umeme hivyo hupata joto au kuchoka na huitaji kutulizwa. Maji ni dawa bora zaidi kwa mwili wa binadamu kwa kuwa husaidia kurekebisha joto la mwili na kuondoa uchovu hivyo kufanya kazi vizuri zaidi.

Maji ya Kunywa

Mtu anaekunywa maji mengi, huwa na uwezo mkubwa zaidi wa kufanya kazi sio tu zile za kutmia nguvu lakini pia zile ambazo hutumia akili kwa kiwango cha hali juu cha kuuchosha ubongo. Kutokunywa maji kwa kiwango kinachotakiwa hupelekea uchovu wa haraka, usingizi na kuzubaa pamoja na unyonge wa mwili. Kutokunywa maji mengi husababisha maumivu ya kichwa yasiyo ya lazima.

5. Hupunguza Uzito.

Kunywa maji mengi kunapunguza sana uwezekano wa kula vyakula mara kwa mara. Hii ni kwa sababu mara nyingi watu huhisi wana njaa na kulazimika kula ili kuiondoa njaa hiyo hivyo tumbo kujazwa vyakula wakati wote na kupelekea kuwa na uzito/unene uliopitiliza.

Kunywa maji mengi mara kwa mara kunaondoa hali ya kutaka kula mara kwa mara kwa kuwa mwili unakuwa na nguvu hivyo kuupunguza mwili kwa kiasi kinachotakiwa.

6. Huondoa maumivu ya viungo

Watu wengi wanasumbuliwa na tatizo la viungo vya mwili kupata maumivu au kuchoka sana lakini watu hao bahati mbaya hukimbilia tiba za madawa kabla ya kujiuliza kama wana maji ya kutosha mwilini. Kunywa maji mengi husaidi kuondoa maumivu ya viuongo na kuufanya viungo hivyo kuwa na ulaini unaofaa.

7. Huondoa Uchafu na ‘acid’

Kunywa maji mengi husaidia kusafisha kibofu cha mkojo kwa hali inayofaa. Mwili huondoa kiasi kikubwa sana cha uchafu unaotakiwa kutoka mwilini kwa njia ya mkojo na jasho. Mtu anayekunywa maji mengi hujikuta anatoa maji mengi mwilini yanayotoka na uchafu usiofaa mwilini hivyo kuufanya mwili kuwa katia hali nzuri ya kufanya kazi na kuzalisha virutubisho.

Pia maji husaidia mashine za mwili kufanya kazi kwa kiwango kizuri katika kuchuja na kuchakata vyakula kupata virutubisho. Maji mengi husaidia kuondokana na uwezekano wa kuvimbiwa.

8. Husaidia matunzo bora ya ngozi

Ngozi huchukua sehemu kubwa zaidi ya miili yetu hivyo ni eneo ambalo linapaswa kuangaliwa na kupewa matunzo ya hali ya juu. Kunywa maji kwa wingi kunasaidia ubora wa ngozi na kung’arisha rangi ya ngozi husika kwa kiwango kinachotakiwa. Inasaidia pia katika kujenga zaidi seli za mwili.

Hizo ni faida chache za Maji katika mwili wa binadamu ambazo zinakupa sababu zaidi ya kunywa maji mengi kadri iwezekanavyo. Kwa kawaida unashauriwa kutumia angalau lita mbili na nusu hadi tatu za maji kila siku.

Kiasi hicho cha maji kinaweza kuwa kigumu sana kunywa kutokana na maisha ya mihangaiko ya watanzania wengi. Lakini, ili kukamilisha kiwango hicho kwa faida ya mwili wako, unapaswa kuhakikisha kuwa popote ulipo una uko karibu na chupa kubwa ya maji na unaitumia ipasavyo.

Unapaswa kunywa maji mengi hadi pale utakapoanza kukojoa angalau mara kadhaa na mkojo uwe mweupe sana. Mhimize sana rafiki, mpenzi na ndugu yako kuhusu zoezi la kunywa maji.  Na kwa wana familia, hakikisha mnakunywa maji kwa wingi na inakuwa tabia na taratibu za familia.

Ili kunywa maji mengi zaidi, epuka kunywa maji ya baridi sana. Maji yenye uvuguvugu kidogo au yasiyotoka kwenye majokofu yanapendekezwa zaidi na wataalam wa masuala ya afya kama tiba sahihi ya mwili wa binadamu.

TFF, NHIF Zasaini Mkataba
Jurgen Klopp Aendeleza Misimamo Ya Kukataa Kazi