Zikiwa zimebaki saa chache kabla ya pambano kubwa la masumbwi ya ubingwa wa dunia wa WBO uzito wa welterweight kati ya Jeff Horn na Manny Pacquiao, kambi ya Horn imetamba kuushangaza ulimwengu, kusimamisha pambano kwa ‘knock out’.

Mkufunzi wa Horn, Glenn Rushton amesema kuwa amegundua kambi ya Pacquiao inawachukulia poa, lakini wao watawashangaza na itakuwa ‘alfajiri ya damu za  pacquiao.

“Tunafanyia kazi kila kona. Kama wanafikiri ataenda kurusha ngumi ya mkono wa kulia na kujaribu kufikisha kama alivyofanya Jessie Vagas, haitakuwa hivyo,” alisema Rushton.

“Jeff anaweza kumpiga KO kwa ngumi yoyote. Ni kama vile hatuihitaji KO bali tunaitaka,” aliongeza.

Feff ambaye ni raia wa Australia mwenye rekodi ya kutopoteza pambano hata moja kati ya mapambano yake 17, ameahidi kumnyang’anya Pacquiao mkanda wa ubingwa wa dunia mbele ya mashabiki zaidi ya 55,000 watakaohudhuria pambano hilo nchini Australia.

Pambano hilo lililopewa jina la ‘Battle in Brisbane’ litashuhudiwa kwenye uwanja mkubwa wa mpira wa miguu jiji humo.

Magazeti ya Tanzania leo Julai 2, 2017
Video: Mpina awaka, wanaokaidi kutunza mazingira sasa kuchukuliwa hatua kali