Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amepongezwa kwa namna ambavyo amekuwa mstari wa mbele katika kusimamia rasilimali za Taifa ili ziweze kuwanufaisha wananchi wote.

Pongezi hizo zimetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Good News for All Ministry, Askofu Charles Gadi alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari pamoja na kufanya maombi ya kuzuia kunyesha kwa mvua zenye madhara.

“Napenda kuchukua nafasi hii kwa dhati kabisa kama kiongozi wa dini kumpongeza Rais Magufuli kwa kufanikiwa kusimamia kikamilifu rasilimali za nchi yetu hususan eneo la madini ya dhahabu na vito,hadi kuwezesha kurejeshwa sehemu ya malimbikizo ya kodi ambayo huenda tusingeipata kama siyo jitihada zake,” amesema Askofu Gadi.

Aidha, amesema kuwa kama si ujasiri aliouonyesha Rais Magufuli katika kupigania rasilimali za nchi, kama isingekuwa msimamo wake wa kutoyumbishwa na makampuni ya madini huenda makubaliano yasingefikiwa kama ilivyo sasa.

Hata hivyo, awali akizungumza kabla ya kuanza kuomba kuhusu kuzuia mvua zenye madhara kunyesha kwa lengo la kuokoa maisha ya watanzania wanyonge jambo linaloelezwa kuwa ni hatua nzuri kwa Serikali kuboresha miundombinu. 

Serikali yataifisha ng'ombe 6648 kutoka Uganda
Serikali yazikaba koo kampuni za Bima