Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amekosolewa vikali kwa kusinzia bungeni wakati wa uwasilishaji wa taarifa muhimu ya bajeti ya nchi hiyo.

Zuma alinaswa na kamera akiwa amesinzia wakati Waziri wa Fedha wa nchi hiyo, Pravin Gordhan akiwa anawasilisha bajeti ya muhula mfupi, Jumatano wiki hii.

Uwasilishaji huo wa bajeti ulichukua saa moja na dakika 14 na kurushwa moja kwa moja kwenye vituo vya runinga, licha ya kumuonesha mkuu huyo wa nchi akiwa amesinzia, mambo yote yalikuwa yakiendelea kama kawaida.

Zuma amekuwa akikumbana na changamoto kubwa katika uongozi wake ikiwa ni pamoja na kuamriwa na mahakama kurejesha fedha alizotumia kukarabati nyumba yake binafsi huku akisalimika katika jaribio la kura ya wabunge kumuondoa madarakani.

Sumaye afunguka kuhusu kunyang’anywa shamba, 'CCM wasahau, sirudi Ng’o'
Yanga Yamgeuka Lwandamina, Yamrudisha Babu Pluijm