Uswizi imeripotiwa kuidhinisha matumizi ya kifaa cha kujimalizia (kijiua) kiitwacho” Sarco capsule”. 2022

Inasemekana kifaa ukitumia unaaga dunia ndani ya sekunde 30 tu, kinakufanya unakufa kwa amani kabisa kama umelala kwa mujibu wa maelezo ya Dr Nitschke

Ukiingia humo kuna maswali kadhaa ambayo yamerekodiwa utayajibu halafu wewe ndie unae bonyeza kitufe kwa ndani ili kujiua, na unaweza kuipeleka eneo lolote la kujiulia, kama ni nje au ndani.

Ukibonyeza kitufe mle mdani, Nitrojeni inajaa ndani na kusababisha oksijen kuwa chini kutoka asilimia 21 hadi asilimia 1 ndani ya sekunde 30 tu na kupoteza fahamu.

Kifo hutokea kutokana na hypoxia (oksijeni kuwa chini katika tishu za mwili) na hypocapnia (kupunguzwa kwa kabon daioksaid katika damu).

“Faida kwa mtu anayeitumia ni kwamba hawahitaji kupata ruhusa yoyote, hawahitaji daktari maalum kujaribu kuingiza sindano, na hawahitaji kupata dawa ngumu,” alisema Dr. Nitschke ambae ndie mgunduzi wa Sarco Capsule alipokuwa akitoa maelezo ya kifaa hicho.

Sarco imetengenezwa na shirika lisilo la faida la kimataifa la “Exit International” lenye makao yake makuu Australia.

Takriban watu 1,300 walikufa kwa kusaidiwa kujiua nchini Uswizi mnamo 2020 kwa kutumia huduma za mashirika makubwa zaidi ya kusaidia kujiua nchini humo, Exit na Dignitas, kulingana na ripoti ya SwissInfo.

Hivi sasa, kujiua kwa kusaidiwa nchini Uswizi kunamaanisha kumeza tembe iliyojazwa aina ya vitu ambayo humfanya mtu awe katika hali ya kukosa fahamu kabla hajafa.

Watu husaidiwa kujiuwa kama familia zao zikikubaliana aidha kutokana na mateso ya maumivu makali ya magonjwa kama kansa na yale yasiyotibika au mtu mzima sana ambae haoni sababu ya kuendelea kuishi na sababu zingine.

DC Longido atoa maagizo katika halmashauri
Simba SC yarejea Dar es salaam