Jitihanda za kuzuia maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi nchini zimeendelea kupata changamoto kubwa huku tafiti zikionesha kuwepo kwa maambukizi makubwa kwa wanawake wanaojihusisha na biasharaya kuuza miili yao.

Utafiti uliofanywa hivi karibuni na Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na upimaji wa Virusi Vya Ukimwi la ‘Tumaini’, umeonesha kuwa wanawake wanne kati ya kumi wanaofanya biashara ya kuuza miili yao wana vizuri vya ukimwi.

Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Onesmo Mwihava ameviambia vyombo vya habari kuwa matokeo ya utafiti huo yanatokana na vipimo walivyokuwa wakiwafanyia watu mbalimbali katika maeneo ya starehe na madanguro. Alisema kuwa mbali na virusi vya ukimwi, wengi wamekutwa na magonjwa ya zinaa.

Kutokana na matokeo hayo, Onesmo ameitaka Serikali na vyombo vingine kuhakikisha vinaongeza juhudi katika kupambana na biashara haramu ya ngono nchini ili kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Rais Wa Uganda Athibitisha Kuguswa Na Msiba
Babu Wa Young Africans Aanza Kuvuta Harufu Ya Ugumu Wa Al Ahly