Wakati harakati za kampeni za uchaguzi wa Kenya zikiendelea, utafiti uliofanywa na shirika la African Electoral Observation Group umeonesha kuwa endapo uchaguzi huo ungefanyika leo, Rais Uhuru Kenyatta (Jubilee) angeibuka mshindi dhidi ya Raila Odinga (NASA).

Utafiti huo uliowasilishwa ikiwa zimebaki takribani siku 60 kabla wananchi wa taifa hilo kufanya maamuzi kupitia sanduku la kura, umeonesha kuwa takribani asilimia 89 ya wapiga kura watajitokeza kushiriki uchaguzi huo, sawa na watu milioni 16 kati ya milioni 19.2 ya wapiga kura wote waliojiandikisha.

Matokeo ya utafiti huo yameonesha kuwa Rais Kenyatta angeshinda kwa takribani asilimia 51.7 dhidi ya Odinga ambaye angepata asilimia 39 ya kura zote.

Mwaka 2013, Rais Kenyatta alimshinda Odinga kwa tofauti ya kura 800,000, akipata ushindi kwa asilimia 50.51 tu. Zaidi ya asilimia 86 ya wapiga kura wote walishiriki uchaguzi huo, sawa na wapiga kura milioni 12.3.

African Electoral Observation Group wameeleza kuwa maeneo ambayo yanadaiwa kuwa ni ngome ya Jubilee yanatarajiwa kuwa na wapiga kura wengi ukilinganisha na maeneo yanayochukuliwa kama ngome ya NASA.

Picha: Messi alivyofunga ndoa ya kifahari na rafiki yake wa utotoni
Tume ya uchaguzi Kenya yajibu kuhusu 'marehemu kupiga kura'