‘Kujamiiana’ ni kitendo hatari sana kwa maisha ya binadamu yoyote endapo kitendo hicho kitafanywa bila kuzingatia ‘kinga’ zinazofaa, lakini ni tendo linaloweza kuleta raha na afya nzuri endapo litakuwa katika hali salama, ya maridhiano na inayozingatia kiasi.

Kinga katika kujamiiana inaweza kuwa ni kutumia ‘kondomu’ au kushiriki na mtu mwaminifu na salama kwako baada ya kupata vipimo vya pamoja na mkawa ‘buheri wa afya’.

Hata hivyo, kutokana na raha ya tendo lenyewe na ushawishi wake, watu mbalimbali wamekuwa wakijiuliza je, ni mara ngapi kiafya inaweza kuwa vyema zaidi kushiriki tendo hilo na je, ni mara ngapi kunaweza kuwa ni hatari kwa afya yako?

Katika kujibu swali hili, watafiti wengi walifanya kazi ya kutafuta majibu huku wakiweka msisitizo kuwa kila kinachozidi ni ‘sumu’ na kila kinachopungua kinaweza kuleta ‘udhaifu’ fulani.

Profesa Laurie B. Mintz wa Chuo Kikuu cha Florida, alifanya utafiti na kuandika katika kitabu chake cha ‘A Tired Woman’s Guide to Passionate Sex’ utafiti ambao muhtasari wake ulichapishwa na shirika la Planned Parenthood federation of America.

Katika utafiti huo, aliwahusisha wanafunzi zaidi ya 100 wa chuo hicho wenye umri kuanzia miaka 21 na kuendelea.

Original 3

Profesa Mintz alibaini kuwa wale ambao walikuwa wanajamiiana mara moja au mara mbili tu kwa wiki walikuwa na asilimia 30 zaidi ya virutubisho vya ‘immunoglobulin A (IgA) kuliko wale ambao walikuwa hawafanyi kabisa au wale ambao walikuwa wanafanya mara kwa mara au zaidi ya mara mbili kwa wiki.

“Kwa kuwa IgA ni muhimu sana katika kinga za mwili wa binadamu, inaonekana kuwa kwa mujibu wa utafiti huu mdogo, wanafunzi wanaotaka kufaidika zaidi na jinsi ambavyo kinga za mwili wao zinafanya kazi wanapaswa kufanya mapenzi mara moja au mara mbili tu kwa wiki,” alisema Profesa Mintz.

Pia, Profesa Mintz alikinukuu kitabu cha Yvyonne Fulbright (Link is Exeternal), kinachohusu madhara ya kufanya mapenzi kupita kiasi na kueleza kuwa ni hatari kwa afya ya binadamu yoyote.

Kadhalika, Profesa huyo alipokuwa akiwasilisha majibu ya tafiti zake kwa wanafunzi wake aliwaeleza kuwa hakuna namba sahihi zaidi katika maisha yako kuhusu mara ngapi ufanye mapenzi lakini ni tatizo kubwa zaidi pale unapojikita katika kufanya mapenzi na yakafikia hatua ya kuanza kuingilia shughuli zako za kila siku.

Profesa Mintz aliwasisitiza watu wote kuhakikisha kuwa wajamiiana katika hali ya usalama kiafya kwa hali yoyote waliyonayo na kwa yeyote wanaetaka kufanya naye tendo hilo.

 

Lionel Messi Ameanza Mdogo Mdogo
Game Ya Ubelgiji Vs Hispania Yaota Mbawa