Utafiti uliofanywa kupitia takwimu za Idara ya Takwimu ya Taifa ya Uingereza kuhusu hali ya uzazi nchini humo umebaini kuwa wakati wa sikukuu za Christmas ndio wakati ambao mimba nyingi zaidi hutungwa kuliko kipindi kingine chochote katika mwaka.

Utafiti huo uliotumia takwimu za kuanzia miongo miwili iliyopita kutoka katika idara ya Taifa ya Takwimu zimeonesha kuwa mimba nyingi zaidi hutungwa siku ya Christmas,  siku chache kabla ya sikukuu za Christmas na siku chache baada ya sikukuu hizo. Hayo yamebainika kutokana na idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa  mwezi Septemba (miezi 9 baadaye).

“Kwa kawaida jumla ya watoto 1800 huzaliwa kila siku, lakini idadi hiyo huongezeka hadi kufikia watoto 1,974 ifikapo Septemba 26 kila mwaka,” Idara hiyo ya Takwimu ya Taifa imeeleza.

Imeelezwa kuwa hiyo huchangiwa na ukweli kwamba katika kipindi hicho cha sikukuu za Christmas, wanafamilia wengi hujumuika pamoja na wanandoa hua katika hali ya furaha zaidi ya mapumziko.

“Wazo kwamba mimba nyingi hutungwa wakati wa Krismasi lina msingi. Nina uhakika sherehe na shamra shamra za wakati huu huchangia,” alisema Profesa wa Chuo Kikuu cha Sheffield Allan Pacey.

Ridhiwani Afunguka Kuhusu Tuhuma Za Ufisadi na Uhusika Sakata la Makontena
Rais Amuokoa Mwanaume Aliyetaka Kujiua kwa Kujirusha Kutoka Darajani