Moja kati ya changamoto kubwa  inayoikabili dunia hivi sasa, ni tatizo la kuzorota kwa ufanisi katika utungaji mimba ili kufanikisha agizo la Mwenyezi Mungu, “Zaeni Mkaongezeke”.

Tatizo hilo kwa asilimia kati ya 40 hadi 50, kwa mujibu wa tafiti za kisayansi linasababishwa na wanaume kutokuwa na mbegu bora zenye ufanisi ikiwa ni pamoja na tatizo la nguvu za kiume.

Katika kutafuta suluhisho, mengi yamefanywa na watafiti na kubainika kuwa ulaji, unywaji na uvutaji ni chanzo kikuu cha tatizo hilo. Utafiti uliofanywa hivi karibuni na wanasayansi nchini Marekani umebaini kuwa njugu zinaweza kusadia kuboresha mbegu za kiume na kuongeza nguvu za kiume.

Watafiti hao, katika kutafuta majibu ya matokeo ya njugu, liliwatumia wanaume 119 wenye umri kati ya miaka 18-35. Watafiti hao waliwagawa wanaume hao katika makundi mawili, kundi moja la wanaume walikula njugu gramu 60 kwa siku kwenye mlo wao. Halafu kundi lingine halikujumuisha njugu kwenye mlo wao.

Baada ya wiki moja, walibaini kuwa wanaume ambao walikula njugu, mbegu zao za kiume ziliboreka kwa asilimia 14 na pia nguvu zao za kiume ziliongezeka kwa asilimia 4.

Kadhalika, mwendo kasi wa mbegu zao za kiume uliongezeka kwa asilimia sita huku umbo nalo likiongezeka kwa asilimia moja.

Imeelezwa kuwa endapo mwanaume atakuwa anakula njugu ujazo wa kiganja kimoja tu kwa siku, baada ya siku saba ataona matokeo mazuri kwenye afya yake ya uzazi.

Kwa bahati nzuri, njugu zinapatikana kwa wingi barani Afrika, chukua hatua boresha afya ya uzazi. Kumbuka uvutaji sigara na ‘ulevi’ wa pombe vinatajwa kwa kiasi kikubwa kuzorotesha ubora wa mbegu za kiume.

Ruto ajibu utafiti unaoonesha anatajwa kuongoza kwa rushwa
Makamba aagiza uanzishwaji wa kamati za mazingira