Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimefanya utafiti ambao umeonyesha kuwa wafanyakazi wengi hawalipwi malipo ya likizo huku baadhi ya waajiri wakiwalazimisha wafanyakazi kuuza likizo zao ili walipwe malipo hayo.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Ofisa Msaidizi Kitengo cha Haki za Binadamu na Biashara, Tito Magoti, wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Utafiti wa Haki za Binadamu na Biashara ambapo amesema hali hiyo inaonyesha jinsi gani wafanyakazi wengi hawaelewi haki zao.

Amesema kuwa tatizo hilo limeonekana kuwa kubwa zaidi katika mikoa ya Morogoro na Mwanza na kwamba utafiti huo umeonyesha kuwa ni asilimia 13 pekee ndiyo wanaofahamu haki zao mahala pa kazi.

“Utafiti huu pia umebaini kuwa wafanyakazi wengi hawapati nafasi ya kujumuika ikiwamo kujiunga na vyama mbalimbali vya wafanyakazi,”amesema Magoti

Ospina asitisha usajili wa Mignolet SSC Napoli
Chadema yakanusha kuhusu Lowassa kugombea Monduli