Hivi karibuni, utamaduni wa kuchora ‘Tattoo’ mwilini umezidi kuongezeka. Baadhi huchora michoro hii kwa kuweka kumbukumbu fulani, au kuonesha misimamo fulani huku wengine wakichora kwa ajili ya urembo tu.

Utafiti uliofanywa na Professor Viren Swami wa Chuo Kikuu cha Anglia Ruskin, iliyoko Cambridge, Uingereza umebaini kuwa watu wenye ‘tattoo’ mwilini huwa na tabia za hasira na ukali kuliko wale ambao hawana.

Profesa Viren alitumia sampuli yake ambayo iliwajumuisha watu wazima 878 kati yao wanaume 197 na wanawake 181, wenye umri kati ya 20 hadi 58.

Kati ya watu hao, watu 97 walikuwa na michoro ya tattoo miilini mwao, ambao ni wastani wa mtu mmoja kati ya watu wanne katika sampuli yake.

Katika ufafanuzi wake, Profesa Viren alieleza utafiti wake umebaini kadri mtu anavyozidi kuongeza tattoo mwilini mwake ndivyo anavyozidi kuongeza hali ya kuwa na hasira. Aliongeza watu wengi wenye tabia ya kuyabeba kichwani kwa muda mrefu matukio yaliyowaumiza au kuwakatisha tamaa huamua kuchora tattoo ya kumbukumbu.

Wachezaji Wa Simba Wavamiwa
Baada ya Kuadhibiwa, Mourinho Atoa Ya Moyoni