Taasisi ya kimataifa inayochunguza masuala ya rushwa na ubadhirifu, Transparency International imetaja ukanda wa Jangwa la Sahara – Afrika kuwa ndio wenye nchi zinazoongoza kwa rushwa katika sekta ya umma.

Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti uliofanyika mwaka jana, Somalia, Syria na Sudan Kusini ndizo nchi zinazoongoza duniani kwa rushwa katika sekta ya umma. Imeeleza kuwa nchi nyingi zinazokabiliwa na rushwa kwa kiwango kikubwa hazioneshi jitihada za dhati za kukabiliana nayo.

Utafiti huo umeweka kiwango cha 100 kuwa kiwango cha juu zaidi cha kutokuwa na rushwa na 0 kuwa ndiyo kiwango cha juu zaidi cha rushwa katika nchi husika, ikizigusa nchi 180 duniani kote.

Wakati Sudan Kusini, Syria na Somalia zikiongoza kwa kuwa na kiwango cha juu cha rushwa, Denmark na New Zealand zimeongoza kwa kuwa na kiwango cha chini zaidi cha rushwa katika nchi zilizopitiwa. Denmark ilipata alama 88 na New Zealand ina alama 89. Syria ina 14, Sudan Kusini ina 12 na Somalia ina 9.

“Eneo lenye kiwango kizuri zaidi ni Ulaya ambayo ina wastani wa 66. Eneo ambalo lina hali mbaya zaidi ya rushwa ni ukanda wa Sahara Afrika wenye wastani wa alama 32,” imeeleza ripoti hiyo.

Wafanyakazi wa ndani waandamana kudai haki zao
Polisi yakana kuhusika kukamatwa kwa mwandishi wa habari