Klabu ya Young Africans ambayo kwa sasa haipo vizuri kifedha kufuatia mwenyekiti wao Yusufu Manji, ambaye pia alikuwa mfadhili kupata matatizo, huenda ikaingia mkataba na kampuni SportsPesa ya nchini Kenya.

Kampuni hiyo imeonyesha nia ya kutaka kuwekeza kwa mabingwa hao wa soka Tanzania bara, kwa kusaini mkataba wa miaka mitano, wenye thamani ya Billion 4.5, ambao kwa mwaka ni sawa na Shilingi milioni 900.

Uongozi wa Young Aficans jana ulikutana na wawakilishi wa kampuni hiyo, ambapo wakikubaliana kuingia mkataba wa miaka mitano ambao kila mwaka utakuwa na nyongeza ya asilimia sita ya fedha. Asilimia sita ya milioni 900 ni milioni 54 Kwa hiyo Young Africans watakuwa wanaongezewa million 54.

“Wawakilishi wa SportPesa watakutana na uongozi wa Young Africans ili kumalizana nao juu ya mkataba wanaotaka kuingia na hiyo ni kutokana na kufika makubaliano ya kimkataba,” Alisema mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo.

Alipotafutwa Katibu Mkuu wa Young Africans, Charles Mkwasa, alisema ni kweli wapo kwenye hatua za mwisho za kuingia mkataba na SportsPesa.

“Napenda nizungumze kitu kilichokua tayari au kimekamilika hatua ya kuingia mkataba na SportsPesa bado, ila tutakutana nao kwa mazungumzo ya mwisho ambayo yatatoa jibu kama watatudhamini au la.

“Tunazungumza na SportsPesa kwa kuwa wamekuja moja kwa moja kwetu tofauti na kampuni nyingine ambazo zinataka kutudhamini, lakini ipo kampuni tuliyoipa jukumu la kufanya mazungumzo nao na sisi kutuletea taarifa ya kila kinachoendelea.” Alisema Mkwasa.

Iwapo Young Africans watamalizana na kampuni SportsPesa ya Kenya Itakuwa klabu inayolipwa vizuri Africa Mashariki. Kwa Tanzania mikataba ya awali waliyosaini Simba na Young Africans na kampuni ya bia (TBL) walikuwa wanapewa milioni 500 kwa mwaka, lakini kwa Azam FC wanapata Bilioni 1 Kwa mwaka kupitia Benki ya NMB.

Kampuni ya SportsPesa ndio mdhamini wa klabu ya Hull City inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini England.

Video: Mwakyembe asema ni kazi ngumu kumsafisha Lowassa kuhusu Richmond
Video: Sakata la Richmond laibuka upya, Uhai wa Ben Saanane utata