Serikali imesema kuwa itawapandikiza Sokwemtu katika hifadhi ya Taifa ya Rumanyika Orugundu iliyopo wilayani Karagwe na Ibanda iliyopo Kyerwa, mkoani Kagera kwa kuwa hifadhi hizo zina Ikolojia na chakula cha kutosha kinachoruhusu kustawi kwa Wanyamapori hao hatua itakayochangia kukuza shughuli za utalii wa Sokwemtu hapa nchini na kuongeza pato la Taifa.

Hayo yamesemwa mkoani Kagera na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati wa ziara yake ya Kikazi ya kukagua maendeleo ya shughuli za uhifadhi katika hifadhi hizo zilizotangazwa hivi karibuni kuwa hifadhi za Taifa  na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Dkt. Kigwangalla amesema kuwa mpango huo umekuja kufuatia taarifa za kitaalam zinaonyesha kwamba katika miaka mingi iliyopita kulikuwa na Sokwemtu katika maeneo hayo ya wilaya ya Kyerwa na Karagwe ambayo watalaam wanasema ikolojia yake inaruhusu kustawi kwa Wanyamapori hao kwa kuwa yana makazi mazuri na chakula cha kutosha.

Dkt. Bashiru atoboa siri ya kumpokea Ole Millya ndani ya CCM
Waratibu wa dawati la 'Afya Moja' kutekeleza dhana ya Afya Moja