Jeshi la Polisi nchini limewatadhadharisha wananchi juu ya uwezekano wa kuibuka kwa matapeli baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi kutoa tangazo la ajira Desemba mosi, 2022 kwa vijana wenye sifa za kuajiliwa na Jeshi hilo.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), David Msime alipotoa taarifa kwa vyombo vya habari kufuatia kutangazwa kwa nafasi za ajira za Polisi alisema vijana, wazazi ama walezi wasikubali kurubuniwa na mtu yeyote kuwa anao uwezo wa kukusaidia kupata ajira hizo nje ya utaratibu uliotangazwa.

Misime ameongeza kuwa, Jeshi la Polisi linasisitiza kama kijana anazo sifa zilizoainishwa katika tangazo la ajira ni vema akafuata maelekezo yaliyoambatana na tangazo hilo na si vinginevyo.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), David Msime.

Amesema, “Ukikiuka na kufuata maneno ya ulaghai wa matapeli watakao kuambia toa kitu fulani ili usaidiwe, itakuwa ni hasara kwako na hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yako kwa mujibu wa sheria pamoja na tapeli mhusika,pale itakapo bainika” alisema Misime.

Hata hivyo, Jeshi hilo limetoa wito kwa wananchi kutoa taarifa pale watakapo baini kuibuka kwa watu (matapeli), wa aina hiyo ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Picha: Mwenyekiti wa CCM ashiriki zoezi la kupiga kura
Petroli yashuka, Dizeli yapaa: EWURA